Pages

Friday, August 17, 2012

MISS KARUN WA CAMP MULLA BADO NI BIKIRA


Wanaume wa Kenya wanaommendea first lady wa Camp Mulla, Miss Karun, inabidi wajiandae kukutana na mama yake ambaye ni mkali zaidi ya mbogo!

Inadaiwa kuwa japo Miss Karun ameshauvuka umri wa hatari unaoweza kumpeleka kidume jela kama akila 'tunda' lake, mama yake hamruhusu kuwa na mpenzi.

Mama yake ni wale akina mama ‘wakoloni’ na matajiri ambaye hawezi kumruhusu mwanae huyo mrembo aende kwenye concert na kukosa masomo, hata kama inalipa kiasi gani!


Anasoma kwenye shule yenye gharama nchini Kenya iitwayo Braeburn.

Inadaiwa kuwa mama yake humchagulia hadi nguo za kuvaa. Siku ya fainali ya Tusker Project Fame mwezi uliopita ambapo Camp Mulla waliperform alivaa nguo ambazo mama yake hakuzikubali.

Inasemekana kuwa aliporudi nyumbani alichezea kichapo cha paka mwizi na kuambiwa kuwa siku nyingine akiperform anatakiwa aufunike mwili wake kwa kuvaa soksi ndefu ama tight.

0 maoni:

Post a Comment

Labels