Pages

Friday, August 31, 2012

KALALA KUANZA KAZI RASMI LEO HII.

 Kalala akiwa na Kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta Saleh Kupaza siku ya kutangazwa kwake.

Mwimbaji nyota wa muziki wa dansi, Kalala Junior aliyehamia katika Bendi ya African Stars "Twanga Pepeta" Ijumaa hii tarehe 31 mwezi huu anataraji kuanza kazi rasmi katika bendi yake hiyo mpya.

 Akiwa na warembo wa Twanga Pepeta wanaounda safu ya mbele ya wanenguaji.

Kalala ataanzia rasmi kufanya kazi katika ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo katika Jengo la Millenium Tower lililopo maeneo ya Makumbusho Jijini Dar es salaam. 
 
Jumamosi itakuwa zamu ya ukumbi wa nyumbani wa Mango Garden na Jumapili atamalizia Leaders Club Kinondoni mchana kuanzia saa nane.

0 maoni:

Post a Comment

Labels