Pages

Thursday, May 29, 2014

Apple yatangaza rasmi kuinunua kampuni ya Dr. Dre ‘Beats Electronics’ kwa dola bilioni 3

dre-e1399586836803
Confirmed Apple yatangaza rasmi kuinunua kampuni ya Dr. Dre ‘Beats  Electronics’ kwa dola bilioni 3

Baada ya taarifa za uvumi zilizosambaa wiki tatu zilizopita hatimaye kampuni ya Apple imetangaza rasmi kuinunua kampuni ya Beats Electronics na Beats Music za producer mkongwe Dr. Dre kwa dola bilioni 3, kwa mujibu wa Billboard.

May 8 mwaka huu iliripotiwa kuwa Apple inampango wa kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 3.2.

Waanzilishi wa Beats producer mkongwe wa Hip Hop Dr. Dre na mwanzilishi wa Interscope Jimmy Iovine watapewa vyeo vya juu katika kampuni ya Apple, ambavyo hata hivyo havikutajwa moja kwa moja katika tangazo hilo.

Dre na Lovine walinzisha Beats Electronics mwaka 2008 na kwa wakati huo walikuwa wakitengeneza headphones peke yake, lakini kwa sasa pia wana mtandao wa kustream muziki.

Deal ya Apple kuinunua kampuni ya Beats Electronic inatarajiwa kukamilika September 30 mwaka huu.

0 maoni:

Post a Comment

Labels