Pages

Friday, May 30, 2014

MWONGOZAJI WA FILAMU MAARUFU TZ ''GEORGE TYSON'' AFARIKI DUNIA

Kwenye watu ambao wana mkono mkubwa kwenye filamu Tanzania basi na huyu ni miongoni mwao, amehusika kwenye movie nyingi sana zikiwemo za mke wake ambae ni mwigizaji Monalisa kama ile ya ‘Girlfriend’ aliyocheza na kina GK, T.I.D Ay na wengine miaka hiyo.
Screen Shot 2014-05-31 at 1.02.00 AM 
Kuanzia saa tatu usiku wa May 30 2014 zilianza kusambaa taarifa kwamba Director George Tyson amefariki dunia ila sasa ndio zimethibitika kuwa ni rasmi ambapo Mwigizaji Wema Sepetu na mtangazaji Zamaradi Mketema ni miongoni mwa waliopata uthibitisho.

Wema ameandika ‘Kwa mara ya tatu bila kupumzika week tunamzika mwenzetu mwingine George Tyson dah.. sina cha kuongea, RIP Brother, Daah sijui Da Mboni wangu ana hali gani aisee…. pole dada akee Mungu akupe nguvu wewe pamoja na team yote ya The Mboni show, pigo kubwa tena kwa wasanii, tunaisha tu jamani.

Screen Shot 2014-05-31 at 1.02.05 AM 
Alichoandika Mtanagazaji wa Take One ya Clouds TV Zamaradi Mketema.
Screen Shot 2014-05-31 at 1.02.34 AM
Screen Shot 2014-05-31 at 1.02.47 AM 

0 maoni:

Post a Comment

Labels