Pages

Wednesday, May 07, 2014

Cyrill Kamikaze atangaza dili ya laki 5 kupitia single yake mpya ‘Alowa’

Rapper wa kundi la Wakacha Cyrill Kamikaze jana ameachia single mpya iitwayo ‘Alowa’, iliyotengenezwa na Manecky.

Alowa

Sambamba na single mpya Cyrill pia ametangaza dili kama iliyowahi kutangazwa na Mwana FA na AY wakati wanaachia single yao ‘Bila KUkunja goti’ mwaka jana.

Akizungumza kupitia XXL ya Clouds FM jana wakati anautambulisha wimbo huo, Cyrill amesema kwa yeyote anayeweza kubuni style ya kucheza wimbo huo ajirekodi na kumtumia, na atatoa zawadi ya shilingi Laki 5 kwa mshindi.

“kuna laki tano, yaani wewe uwe mzee uwe mlinzi uwe nani as long as unahisi unaweza ukai dance ukatupa hata style hata kutingisha kichwa”.
Alisema Cyrill.

Kama unahisi unaweza kubuni style ya kuucheza wimbo huo jirekodi na umtumie kupitia Whats App namba 0752 968270 kisha mshindi pia atapata nafasi ya kuonekana katika video yake.

Cyril ni msanii mwingine wa Hip Hop ambaye ameamua kubadilika katika wimbo wake mpya na kuja na mtindo aliosema umetokana na mdumange pamoja
na mduara.

Ameongeza kuwa ameamua kubadilika katika wimbo huo kutokana na sababu mbili moja wapo ikiwa ni kibiashara zaidi, sababu alisafiri kwenda Uganda pamoja na Kenya kujaribu kuwasikilizisha wadau wa muziki ambao walimpa majibu yanayoashiria wimbo utafanya vizuri, hivyo ameamua kuwekeza pesa nyingi katika wimbo huo. 

“hii ndio track yangu ambayo ntaenda kuweka hela nyingi sana, nikimaanisha nataka nifanye video nzuri, ntataka nifanye promotion ambayo itakuwa inaeleweka”. Alisema.

CHANZO:-BONGO5.COM

0 maoni:

Post a Comment

Labels