Pages

Friday, May 16, 2014

KIM KARDASHIAN NA KANYE WEST SASA KUFUNGA NDOA YAO ITALI NA SIO UFARANSA

Imeelezwa kuwa Kim Kardashian na Kanye West wamebadili eneo watakalofungia ndoa yao kutoka Paris Ufaransa na sasa watafunga ndoa hiyo Florence, Italia May 24.
 http://www.imnotobsessed.com/wp-content/uploads/kim-kardashian-kanye-west-526.jpg
Chanzo cha karibu na wanandoa hao watarajiwa kimeiambia ET kuwa wawili hao wamepanga kula chakula cha usiku na wageni huko Paris, Ufaransa kabla ya ndoa na baadae watawasafirisha wageni wote waalikwa kwa ndege binafsi kuhudhuria sherehe ya ndoa yao huko Italia.

Jumamosi, familia ya Kardashians ilimfanyia Kim K ‘bridal shower’ huko Baverly Hills, California.

Hivi karibuni kupitia twitter, Kim K alikanusha habari kuwa wameshafunga ndoa ya kisheria na kwamba bado orodha ya wageni waalikwa haijawekwa wazi na inayoonekana sio ya kweli. 

Alizikana pia picha za shela zinazooneshwa na kuaminika kuwa ni shela atayoivaa. 
 
Kim Kardashian na Kanye West walikuwa katika uhusiano wa mapenzi tangu mwaka 2012 na walichumbiana October 2013.

0 maoni:

Post a Comment

Labels