Kundi la Weusi
linaloundwa na Rappers watano kutoka Arusha [Nikki wa II,Joh
Makini,G-Nako,Bonta Maarifa]lilitajwa kuwa kundi bora la muziki wa kizazi kipya
katika KTMA 2014.
Msemaji wa kundi
hilo Nikki wa Pili amesema kundi hilo sio tu ni kundi bora la hip hop Tanzania
bali ni kundi bora la hip hop Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa kwao
kupata au kutopata tuzo lengo lao ni kupiga hatua mbele kila mwaka na kuvuka
mipaka ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Wimbo wa Nikki wa
Pili ‘Nje ya Box’ aliowashirikisha Joh Makini na G-Nako ulishinda tuzo ya wimbo
bora wa hip hop katika KTMA2014.
Lakini pia kunamzigo
mwengine mpya kutoka kwa Nikki wa II kutoka kwenye kundi la Weusi, na sasa
anasema "Staki Kazi" ndani
yake kuna vionjo vya RnB akiwa amemshirikisha Ben Pol pamoja na G-Nako huku
ngoma ikiwa imetengenezwa na Nahreel wa Switch
Records Joint hiyo itadrop town Tarehe 13.05.2014.
0 maoni:
Post a Comment