Pages

Friday, May 16, 2014

Mzungu Kichaa atambulisha EP yenye nyimbo nne aliyofanya Ulaya na wasanii wa Tanzania

Mzungu Kichaa ambaye anaweza kuimba vizuri pia kwa lugha ya kiswahili ametambulisha Extended Play yake yenye nyimbo nne leo katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm.
Mzungu Kichaa atambulisha EP yenye nyimbo nne aliyofanya Ulaya na wasanii wa Tanzania

Mwimbaji huyo ameeleza kuwa EP hiyo imefanyika barani Ulaya lakini ametumia wasanii wa Tanzania katika kuimba na kupiga vyombo live walipokuwa studio.

Amesema tayari ameingia mkataba na mashirika yanayouza muziki kwa njia ya mtandao na kwamba itaanza kupatikana kwene iTunes, Amazon na njia nyingine.

Kati ya nyimbo nne zinazounda EP hiyo, zipo Tother as One, Relax Your Mind ambayo iko katika mahadhi ya reggae na Hold On.

0 maoni:

Post a Comment

Labels