Pages

Thursday, May 08, 2014

HII NDIYO MAANA YA WIMBO MPYA WA VICTORIA KIMANI "PROKOTO" ALIOWASHIRIKISHA DIAMOND NA OMMY DIMPOZ

Mwimbaji wa label ya Chocolate City, Victoria Kimani amewashirikishwa Ommy Dimpoz na Diamond kwenye wimbo wake anaotarajia kuuachia May 14, unaitwa bokodo ‘Prokoto’.

Wakali hao wameutengeneza wimbo huo kwa kuunganisha lugha mbili ambazo ni Kiswahili na Kiingeza ili kutengeneza kitu ambacho Kinaweza kuwashika mashabiki wao kwa ujumla.

Prokoto haina maana ila ni neno tu la kutunga ambalo limetumika kama alivyozoea kufanya Dully Sykes kwenye nyimbo zake nyingi.

“Prokoto ni jina la kubuni tu ambalo itakuwa style mpya ya uchezaji, watu wataona itakavyotoka video ambayo tunatarajia kushoot very soon.” Ommy Dimpoz alifunguka.

Ommy Dimpoz ameeleza kuwa ‘Prokoto’ ni wimbo mkali sana wa kuchezeka ambao anaamini kwa kutumia lugha hizo mbili wimbo huo utaishika Afrika nzima.

Victoria Kimani yuko Tanzania na inawezekana akawa anaendelea na mchakato wa kushoot video ya Prokoto..

0 maoni:

Post a Comment

Labels