Baada
ya takriban miaka miwili kupita toka Khalid
Mohamed a.k.a TID kuandika barua ya kujitoa na kutotaka kuhusishwa na
Tuzo za
muziki za Kili, leo hii hit maker wa ‘Zeze’ amesema anataka kumaliza
tofauti
zake na waandaaji wa tuzo hizo ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa
msanii
bora kwaajili ya nchi yake.
“I
Really want to Finish My Differences
with Kili Music Awardz so I can Pursue My Dream of becomin a better
Artist for
my Country”. Aliandika Top in Dar katika facebook page yake leo.
Ifuatoyo
ndio barua aliyoiandika
TID wakati anajitoa katika tuzo hizo mwaka 2010:
“Naomba
radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka
pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye
hiki
kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka
kwangu
kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za
msingi:
1.Kwanza
nahisi mimi kama TID na mziki
ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo
hizi
sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao
unakubalika
sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki
hiyo
naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia
nilidhani labda ni upungufu wa mawazo
ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi
fulani
nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine
ambao uko
nao kwenye same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili
kutokana
na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi
sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini
nisiwe
mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango
vya
juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!
3.Kwa
sababu hizi ambazo mimi naona kwangu
hazinijengi sioni sababu ya kuwepo kwenye TUZO hizi tena kwani sidhani
kama ni
wakati wa kuwaangusha mashabiki wangu ambao natumia muda mwingi na
effort
binafsi bila ya mdhamini kuwaunganisha na muziki wangu basi nisameheni
kama
nimewakosea lakini hainisaidii chochote endeleeni na hao mnaowapa kila
category
i will never stop making good music for my country surely i wont,i was
born to
do THIS.”
Siku
za karibuni TID ameonekana kutoa yale
ya moyoni kuhusu watu ambao wamekuwa vikwazo katika maendeleo ya kazi
zake za
muziki, ikiwa ni pamoja na ile story ya kutaka kuumua Alikiba. Na mpya
zaidi
tuhuma za ku copy wimbo wake wa ‘Kiuno’ kutoka kwenye wimbo wa 'Shayman And Petersen - Fendela
Fenduze' wa Zambia.
“Some
FooLs are so Scared with my Sucess
Walisema nataka kuwaua,Now nimecopy this KiuNo song wat is it do u Guys
want
From me bt u so Weak AllaH is Protectin Me!” hii ni status
aliyoiweka jumatatu
wiki hii katika ukurasa wake wa facebook.
Na leotainment
0 maoni:
Post a Comment