Pages

Friday, October 19, 2012

MSANII MWINGINE AJITOA KATIKA TUZO ZA KISIMA KENYA

Size 8
Siku chache baada ya DNA kutangaza kujitoa katika Tuzo kubwa nchini Kenya, msanii mwingine wa kike nchini humo anayefanya poa na ngoma ya 'Fire' amejitoa katika tuzo hizo.
 
Gazeti moja  la Kenya limeandika kuwa msanii huyo alishangaa yeye kuchaguliwa kwenye tuzo hizo wakati hajajiandikisha,Size 8 anasema kuwa amejitoa katika Tuzo hizo lakini si kwa nia mbaya, msanii huyo alichaguliwa katika kipengela cha 'Boomba Song of the Year'.
 
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika November mwaka huu ambapo pia baadhi ya wasanii kutoka Tanzania kama Ay, Lady Jayde,Daimond,Chege na Profesa Jay wamechaguliwa kuwania tuzo hizo.

0 maoni:

Post a Comment

Labels