Pages

Monday, October 22, 2012

IZZO AMEKANUSHA UVUMI KUHUSIANA NA KURUDISHWA MBEYA

Hip Hop Icon kutoka The Green City simwingine ni Izzo B amekanusha uvumi ambao umeandikwa kwenye mitandao kwamba mara baada ya kuachia track ya "Utarudishwa" aliyo mshirikisha mkali wa nyimbo za mapenzi kutoka Morogoro Belle 9 kwamba kuna mtoto wa kigogo serikalini amejitokeza na kuandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba "Izzo utarushwa Mbeya kweli"

Akipiga stori kwenye 970 show ya Redio Kitulo Fm na Ergon Elly Izzo amesema hizo nistori tu na aliposikia kuhusiana na ishu hiyo alionahainahaja kufuatilia



Inasemekana Wiki iliyopita, mtoto wa kigogo mmoja serikalini (jina tunalo), aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa kijamii, Facebook kuwa Izzo Business tutakurudisha Mbeya.Baada ya Izzo kuona meseji hiyo, alianza kuzungumza na marafiki zake kwa hisia kwamba baada ya kutoa wimbo huo, zipo njama za kumfanyia kweli..

Baada ya kutonywa na rafiki wa Izzo, iliamua kuzungumza moja kwa moja na mhusika ambaye alijibu hivi: “Ni kweli hii imetokea, nimejaribu kuwataarifu marafiki zangu kadhaa kiusalama tu, ila mimi siogopi, muziki wangu ni harakati na mwanaharakati hatakiwi kuogapa.

“Hata nilipoimba Utarudishwa ni kwa sababu najua muziki wangu unagusa maslahi ya watu, kwa hiyo sipendwi na wale ninaowatibulia ila Watanzania wengi wapo na mimi. Huyo mtoto wa kigogo kama kweli amedhamiria kunirudisha Mbeya, hebu ajaribu tuone.”

0 maoni:

Post a Comment

Labels