Pages

Tuesday, May 14, 2013

Angelina Jolie akatwa matiti kuzuia Saratani

Angelina Jolie Mcheza filamu mashuhuri sana duniani,Angelina Jolie amesema kwamba amekatwa matiti yake yote pamoja na kuondoa mfuko wake wa uzazi.

Kwenye taarifa aliyoandika kwenye gazeti la New York Times, Bi Jolie amesema alifanyiwa uchunguzi wa celi zake na kugunduliwa kwamba alikuwa katika hatari kubwa sana ya kupata saratani ya matiti. Ndipo akaamua kukatwa matiti yake mawili.


Angelina mwenye umri wa miaka 37 na mama na watoto sita, alipoteza mamake mzazi kutokana na maradhi ya saratani ya matiti.
Anasema aliandika taarifa hiyo kuwahakikishia watoto wake kwamba hakuwa kwenye hatari ya kupata saratani tena.


0 maoni:

Post a Comment

Labels