Pages

Tuesday, May 07, 2013

LAURYN HILL KWENDA JELA MIEZI MITATU

Ingawa Lauryn amelipa dola 900,000 wikiendi liyopita lakini bado anaenda jela kwa miezi mitatu. Amelipa karibia dola milioni moja kutokana na kodi za nyuma alizokuwa akidaiwa lakini bado mwanadada anakwenda jela limeripoti Associate Press. 

Msanii huyo 1st lady wa kundi la zamani la Fugees amehukumwa kwenda jela miezi mitatu hii leo katika mahakama iliyopo anapoishi Newwark New Jersey Marekani. 

Lauryn Hill alikuwa afungwe miaka mitatu jela lakini hukumu yake imepunguzwa hadi kufikia miezi mitatu, Baada ya kukutwa na kosa hilo la kukwepa kodi kati ya 2005 - 2007. 

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Lauryn Hill kuingia jela na pia anaweza akatoka mapema baada ya mwezi.

0 maoni:

Post a Comment

Labels