Pages

Monday, May 13, 2013

BECKHAM AVUNJA REKODI YA PEKEE

KIUNGO wa David Beckham ameweka rekodi ya kutwaa mataji ya Ligi Kuu na klabu za nchi nne tofauti, baada ya PSG kuifunga Lyon 1-0 na kutwaa ubingwa wa Ligue 1, Ufaransa.

Beckham, ambaye sasa anakuwa mchezaji wa kwanza wa England kutwaa mataji katika nchi nne tofauti, aliingia akitokea benchi, wakati Jeremy Menez alipokifungia bao pekee la ushindi kikosi cha Carlo Ancelotti.

Ubingwa wa PSG hautathibitishwa hadi Kamati ya Nidhamu ya Ligi itakapokutana kuamua kuipokonya pointi au la kufuatia tuhuma za Mkurugenzi wake, Leonardo kumrubuni refa.

0 maoni:

Post a Comment

Labels