Pages

Monday, May 13, 2013

Nakaaya kuja na ‘Utu Uzima Dawa’

Na Elizabeth John

DADA wa mrembo aliyeingia tano bora za mrembo wa dunia 2005 Nancy Sumari, ambaye ni nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Nakaaya Sumari anatarajiwa kuachia ngoma yake mpya hivi karibuni inayojulikana kwa jina la ‘Utu Uzima Dawa’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Nakaaya alisema maandalizi ya ngoma hiyo yamekamilika, kilichobaki ni usambazaji.

“Naamini ngoma yangu itafanya vizuri wakati wowote kuanzia sasa kama ulivyokubalika wimbo wa ‘Mr Politician’ ulionitambulisha vema katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya,” alisema Nakaaya.

Nakaaya aliwaomba mashabiki kumuunga mkono katika kazi hiyo ili kufikia malengo yake katika tasnia ya muziki.

“Ngoma yangu ya ‘Mr Politician’ ilinitambulisha vema katika anga ya muziki, ambapo nilijinyakulia mashabiki wengi, hivyo nina imani mashabiki hao hawajanipotea, naomba wakae tayari kwa ajili ya kazi yangu ninayotarajia kuisambaza katika vituo mbalimbali vya redio hivi karibuni,” alisema.

0 maoni:

Post a Comment

Labels