Roberto Mancini alitwaa kibarua Man City
Desemba 2009 alipotimuliwa Mark Hughes na kuiongoza kutwaa FA CUP Mwaka 2011 na
Ubingwa wa England 2012 lakini mara baada ya Jumamosi kufungwa Fainali ya FA
CUP Bao 1-0 na Wigan kipigo ambacho kinafuatia kupokonywa Ubingwa wao na
Mahasimu wao Man United.
Mara
baada kufungwa na Wigan kwenye FA CUP, Mancini alikurupuka na kuulaumu uongozi
wa Man City kwa kutokanusha uvumi wa Pellegrini, Raia wa Chile, kuja kutwaa
kazi yake.
Hata
hivyo, baadhi ya Wachambuzi huko England wamemponda Mancini na kudai hana haki
ya kuilaumu Man City kwani hata yeye alipoteuliwa kwenda Klabu hiyo Mark Hughes
alikuwa bado Meneja.
Ingawa
Mancini aliiwekea Man City historia nzuri ya kutwaa Kombe lao la kwanza baada
ya Miaka 35 walipotwaa FA CUP na kutwaa Ubingwa wao wa kwanza baada ya Miaka
44, kumaliza Msimu huu kwa ukame kunadaiwa kuwakera Wamiliki Matajiri wa Man
City toka Falme za Nchi za Kiarabu ambao Jumamosi walikuwa Wembley kushuhudia
Timu yao ikitwaa Kombe kwa mgongo wa ‘vibonde’ Wigan lakini wakajikuta chali
baada ya kutunguliwa Bao 1-0 na Kombe la FA CUP kwenda Wigan, Timu ambayo
huenda Msimu huu ikaandika Historia ya kuwa Klabu ya kwanza kutwaa FA CUP na
kushushwa toka Ligi Kuu Msimu huo huo.
0 maoni:
Post a Comment