Pages

Friday, May 31, 2013

Baada Ya Msiba Wa ALBERT MANGWEA, MwanaFA Atoa Tamko Lingine Kuhusiana Na “THE FINEST”

Baada ya kutokea kwa kifo cha ndugu, rafiki yetu marehemu ALBERT MANGWEA … Rapper MwanaFA alitangaza kuahirisha show yake ya THE FINEST iliyokuwa ifanyike kesho.
Leo hii, MwanaFA ametoa tamko lingine kuhusiana msiba huo wa mwanamuziki mwenzie na pia kuhusiana na show yake ya THE FINEST … Hichi ndicho alichoandika …

“Kutokana na Msiba uliotokea wa ndugu yetu Albert Mangwair, Show ya THE FINEST iliyokuwa ifanyike 31.05.2013 imeahirishwa mpaka baada ya mazishi. Kwa kuwa ulifanya booking, utapigiwa simu kupewa tiketi yako/zako kuanzia tarehe 06.06.2013. Tunaomba radhi kwa usumbu uliojitokeza. Ahsanteni.”

0 maoni:

Post a Comment

Labels