Pages

Saturday, June 01, 2013

RATIBA KAMILI YA MAZISHI YA ALBERT MANGWEHA

Taarifa muhimu toka kwa msemaji wa Familia ya Marehemu
Albert Mangweha ambae ni
Kenneth Mangweha ametoa Ratiba Rasmi baaa ya ile ya jana
kusema mwili ulipaswa kuwasili
Tarehe 1 June 2013 alasiri lakini kutokana na Watanzania
waishio nchini South Africa
kuomba Familia ya marehemu nao kupata nafasi ya kuuaga mwili



wa Ndugu albert,aliyefariki
Nchini South Africa Tarehe 28 May.....
Baada ya Familia kuridhia ombi lao walibid kuenga ratiba ya awali
na kuweka kama Ifuatavyo;
Mwili wa marehemu utawasili Siku ya tarehe 2 June na Shirika la
ndege la South Africa,
kisha kuifadhiwa Hospital kuu ya Taifa Muhimbili....
Tarehe 3 siku ya Jumatatu Mwili utawasilishwa Viwanja vya Leaders
Club Maalum kwa
Mashabiki wa Albert Mangweha kutoa Heshima za mwisho kuanzia
saa 3 asubuhi hadi saa 7mchana Shuguli hiyo itafanyika....
Baada ya hapo Familia na Kamati pamoja na wahusika wengine
wataanza safari kuelekea
Morogoro kwaajili ya kupeleka mwili wa Albert
Mangweha kwa maziko....
Tarehe 4 siku ya Jumanne kutakuwa kuna misaa ya kumuombea
marehemu mpaka saa mchana
kutakuwa na chakula cha mchana msiba utakapofikia kwa
mama yake mzazi mangweha,baada ya
chakula midaa ya saa 8 mchana ndio utakuwa muda umewadia
muda wa kushusha mwili wa mpendwa
wetu Albert Mangweha kwenye nyumba yake ya Milele......
Ni Hayo tu kutoka kwa msemaji wa Familia

0 maoni:

Post a Comment

Labels