Pages

Monday, June 03, 2013

SALAMU ZA RAMBIRAMBI TOKA KWA WIZARA YA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO KUTOKANA NA KIFO CHA MANGWEHA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imepokea
kwa mshituko na masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha msanii
wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Albert Mangweha,
aliyefariki huko Afrika Kusini katika hospitali ya St. Hellen akiwa
katika shughuli za muziki, Jumanne tarehe 28 Mei, 2013.



Kifo cha Albert Mangweha ni pigo kubwa kwa fani ya muziki
hapa nchini, na pia kimataifa. Na kutokana na umahiri wake katika
fani hiyo ya muziki wa kizazi kipya hususan aina yake ya uimbaji
ya “Free Style” alikonga mioyo ya wapenzi wake hasa vijana
ndani na nje ya nchi.

Albert Mangweha atakumbukwa na wasanii na wapenzi wa
muziki kwa kipaji na juhudi zake za kukuza muziki hapa nchini.
Serikali inawapa pole ndugu na jamaa wote na kuwaomba
wawe na uvumilivu na subira katika kipindi cha msiba.

Wito wa Serikali kwa wasanii na wananchi kwa ujumla ni
kuendelea kumuenzi kwa yale yote mazuri aliyoyafanya
wakati wa uhai wake.
“Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya Albert Mangweha
mahala pema peponi.”

Imetolewa na
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo
Dkt Fenella Mukangara

0 maoni:

Post a Comment

Labels