Pages

Thursday, June 27, 2013

Muingiliano wa majina ya bidhaa zao ndio chanzo cha ugomvi ambao unawakabili mastaa hawa kwa sasa.

Imefahamika kuwa, Msanii wa muziki Will.i.am ameamua kumfungulia mashtaka msanii na mtayarishaji muziki Pharell Williams kwa kesi ya madai kutokana na hatua ya Pharel kutumia jina la I AM OTHER katika bidhaa zake mbalimbali anazozalisha zikiwemo Mavazi.



Will.i.am amesema kuwa, jina hili na logo vinakaribiana/vinashabihiana/vinafanana kwa karibu nha brand yake ya WILL.I.AM, na msanii huyu amenuia kutumia sheria kumzuia Pharrel kufnya biashara kwa jina I AM OTHER katika bidhaa zake.

Hii ndiyo Brand mali ya Pharell ambayo Will.i.am hakubaliani nayo.

Tayari wanasheria wa Pharell wamekwishajibu mashambulizi kwa kujibu mashtaka haya kwa maandishi kuwa madai ya Wil.i.am hayana msingi wowote.

0 maoni:

Post a Comment

Labels