Pages

Thursday, June 27, 2013

Rekodi ya Chris Brown kupishana maelewano na vyombo vya dola inaendelea kuchafuka, Huu hapa ni msala mwingine ambao unamkabili kwa sasa.

Chris Brown, muda mfupi tu akiwa anakabiliana na tuhuma za kumdhalilisha mtu katika moja ya kumbi za starehe mwishoni mwa wiki, sasa mapya yamemuibukia msanii huyu ambapo sasa imefahamika kuwa amefunguliwa mashtaka ya kusababisha ajali na kukimbia.


Hii ni kutoka tukio la mwezi uliopita ambapo msanii huyu aliripotiwa kusababisha ajali ndogo ya gari dhidi ya mwanamke ambaye kwa mujibu wa mashtaka, staa huyu alikataa kumpatia taarifa sahihi za leseni na bima yake.

Tayari Chris Brown ameshajibu tuhuma hizi kwa njia ya mtandao na kusema kuwa, mwanamke huyu alikuwa anatafuta namnaya kukuza mambo kwa sababu baada ya kumgonga, alisimama na kuelewana naye, isipokuwa mwanamke huyu alikuwa na nia ya kukuza mambo baada ya kugundua kuwa ana-deal na staa mkubwa katika tukio hili.
Msanii huyu amesema kuwa kwa sasa tayari wanasheria wake wanalishughulikia swala hili ambalo ameliita uzushi mkubwa kutokana na gari la kwake na la mwanamke aliyemgonga kutopata madhara yoyote, na pia kutokana na msanii huyu kuonyesha kujali kuchukua muda wake na kuzungumza na adui yake.

0 maoni:

Post a Comment

Labels