Pages

Sunday, June 30, 2013

'' IMANI YANGU HAINIRUHUSU KUTANGAZA NINAPOTOA MISAADA''Mwana FA.


MSANII maarufu wa Hiphop nchini, Khamis Mwinjuma au maarufu Mwana FA,amesema muziki kwake ni kazi na sababu inayomfanya kila siku azidi kung’ara ni ubunifu alionao ambao humfanya kuwa tofauti na wenzake.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii alisema,muziki ni kazi hivyo inabidi kila siku kufikiria vitu mbalimbali ambavyo atawaletea mashabiki wako ili wazidi kumpenda na kumfanya kutochuja katika muziki”muziki ni kazi hivyo mara nyingi nimekuwa najaribu kubuni aina mbalimbali zaa maneno ili niwe tofauti,kama Unanitega,Bado niponipo na mengine mengi tu,ilio tu yawe mapya kwa mashabiki”.

Akielezea historia yake alisema,muziki alianza toka mwaka 1993 ambapo alifanikiwa kuanzisha kundi ambalo lilikuwa linaitwa,Crew Black Skin na katika kundi hilo alikuwa na marafiki zake wawili ambao ni Robilus na Getheerics.

Mwana FA alikutana na marafiki zake hao kipindi wakiwa katika shule ya Umumio Islami High School,kwani wote kwa pamoja walikua wanachukua masomo ya Sience.

Mnamo mwaka 2000 alifanikiwa kutoa nyimbo yake ya kwanza iitwayo”Ingekuwa vipi”ambayo alimshirikisha Juma Mchopanga”Jay Moe”ambayo ilifanikiwa kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa.

Baada ya nyimbo hiyo alifanikiwa kutoa nyingine kama “Mi na mabinti””Show time”,aliyomshirikisha Ambwene Yessaya”AY,Alikufa kwa ngoma,ambayo alikuwa amemshirikisha Judith Wambura”Lady jay Dee”.
Mwana falsafa kwa mara ya kwanza alifanikiwa kupata tuzo ya Kilimanjaro Music Awards mwaka 2003 kupitia wimbo wake wa,Alikufa kwa ngoma,ambao ulichaguliwa kuwa wimbo bora.

Baada ya kupata tuzo hiyo alitoa albamu ya kwanza iitwayo Mwanafalsafani,ambayo alisema ilifanikiwa kufanya vizuri na hivyo kupata hamasa ya kuendelea kufanya Albamu nyingine ambapo mwaka uliofuata mwishoni alitoa Albamu ya Unanitega,ambayo pia mwaka 2006 ilimpatia tuzo ya Albamu bora ya Hiphop.

Mnamo mwaka 2007 pia mwana FA akiwa ameshirikiana vizuri na AY,walifanikiwa kupata tuzo kupitia wimbo wao wa “Habari ndio hiyo”kuchaguliwa kuwa wimbo bora wa mwaka”nilifurahi sana baada ya kupata tuzo,kwani naamini kila kazi mwisho huwa na mshahara,tuzo ni heshima na ilinipa hamasa kwa kiasi kikubwa sana ya kuzidi kuongeza juhudi katika fani hii na kuzidi kuwa mbunifu”.

Mwana FA ambaye alizaliwa mwaka 1984,kwa kushirikianna na rafiki yake wa karibu,Ambwene Yessaya walifanikiwa kutoa Albamu moja iitwayo”Habari ndio hiyo”,ambayo ndani yake kulikuwa na nyimbo kama“Kula kwa macho”waliyomshirikisha msanii kutoka nchini Uganga”Talia”,”Asubuhi”ambayo walimshirikisha Abubakar Katwila “Q chief”,”Fungua champagne”,”Nangoja ageuke”,”Bounce”,na “Umejuaje”.

Mwana FA hadi sasa tayari ana albamu nne ambazo tayari ameshazitoa,ila kwa sasa amesema albamu hazina faida hivyo yeye atakuwa anatoa nyimbo tu na kufanya maonyesho,kwani anaamini kipato kikubwa kipo katika maonyesho”Kwa sasa sina mpango wa kutoa Albamu kwa sababu unajua hailipi,tumekuwa tunaibiwa sana kiasi kwamba mtu unafanya kazi kubwa ila mwisho wa siku faida haionekani”Albamu hizo ni Mwanafalsafani,Toleo lijalo,Unanitega,Habari ndio hiyo.

Akizungumzia mafanikio ambayo ameyapata hadi sasa anasema ni makubwa sana kiasi kwamba hana budi kumshukuru sana mungu kwa alipofikia kwani hakutaraji kama atafika ila pia bado anazidi kumuomba mungu,kila siku azidi kumpandisha juu zaidi ya hapo”Namshukuru sana mungu na wazazi wangu ambao wamenilea ila kwa kweli nawapongeza na kuwashukuru pia mashabiki kwa kuwa bila wao mimi nisingekuwa hapa nilipo”

Akizungumzia kuhusu watu wachache ambao wamekuwa wakihusisha mafanikio yake na kundi la FreemaSon,alisema umefika muda sasa wa Tanzania kuamka na si kwamba kila mtu anayefanikiwa ni kumhusisha na kundi hilo ”nawaomba wa Tanzania wenzangu wabadilike,si kwamba kila mtu anayefanikiwa basi ameingia katika kundi hilo,mimi ni msanii wa zamani sana hivyo mafanikio nastahili,pia ukizingatia kuwa ni msanii ambaye ninakubalika katika jamii”.

Mwana FA alipoulizwa kuwa anaisaidia vipi jamii inayomzunguka hasa wajane na wale watoto wenye ulemavu alisema,huwa anasaidia kupitia mfuko wa Sawasawa Foundation,ambapo hupeleka misaada yake kwa ajili ya kusaidia watoto yatima na wajane”Unajua imani ya dini yangu huwa hainuruhusu kutangaza pale ninapotoa msaada,sababu hiyo ndio maana huwa nakuwa kimya tu,ila nasaidia kupitia mfuko wa Sawasawa Foundation”
“Na malengo makubwa sana,hasa mwaka huu,kwani nimejipanga vya kutosha kuhakikisha nitafanya mambo makubwa kuliko mwanzo,amini nimejipanga vya kutosha ili nizidi kuwa juu zaidi”
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels