By Fred Bundala
Hakuna anayebisha kuwa jina la Nisher kutoka Arusha kwa sasa ni kubwa nchini kutokana na kuongoza na kutayarisha video za wasanii wakubwa akiwemo Joh Makini, Belle 9, Mabeste na wengine. Hivi karibuni aliongoza na kuitayarisha video ya G-Nako ya wimbo wake Mama Yeyoo aliyomshirikisha Ben Pol.
Hata hivyo Adam Juma ambaye ni muongozaji na mtayarishaji mkongwe wa video za muziki nchini amegundua tatizo dogo kwenye video ya Mama Yeyoo na kuchukua muda wake kumpa darasa. Hivi ndivyo alivyomwambia ingawa alitumia zaidi lugha ya fani hiyo ambayo unaweza usiielewe.
“Dude video is ok, stop using that color preset from magic bullet their crushing the black on the picture as a result all thedetails from the skin tone are gone. Another thing is, use a proper monitor from your edit suite to preview you colours for broadcast, don’t just trust these stupid macbook screens over a simple TV set that everyone views videos from. Yes you have talent, groom it to the direction with knowledge and you will surpass anything,” alishauri Adam.
Kutokana na ushauri huo Nisher alijibu: Many Thanx @Adam Juma … points taken boss… I used HDMI LED Monitors to edit and color grade the video… i didn’t use magic bullet to grade the images but only to flatten them some more… I created my own color palates using AE & Yano Moods… the skin tones are not too visible might be because of YouTube codecs during upload… but thanks for checking it out!
Haya ni maoni ya Joel Joseph wa Fresh 12o aliyeguswa na mazungumzo ya wataalam hao wa video za muziki nchini. “Nisher & Adam I love where this is going together you guys speak your own language and you understand each other. Nisher am so happy that you listen and take note of what have been said by Adam. Haba na haba hujaza kibaba right ? step by step you will be there and Adam keep that spirit of yours you have shown the world how kind you are and how talented both of you are. Keep this spirit and we are following yo back for the support and everything that you are doing.”
Hivi karibuni Nisher ataachia video mpya ya mmoja ya wawakilishi wa Tanzania wa shindano la Big Brother Afrika, Feza Kessy ya wimbo wake Amani ya Moyo aliyoiongoza na kuitayarisha.
CHANZO:-http://www.bongo5.com
0 maoni:
Post a Comment