Pages

Thursday, June 06, 2013

HABARI | Mtoto wa Michael Jackson, Paris alazwa hospitali baada ya kujaribu kujiua

Mtoto wa kike wa mfalme wa pop duniani, hayati Michael Jackson, Paris Jackson mwenye miaka 15, jana alipelekwa hospitali baada ya kujaribu kujiua.
Mtandao wa TMZ ulikuwa wa kwanza kuripoti taarifa hiyo na mama mzazi wa Paris, Debbie Rowe, alithibitisha taarifa hizo na kwamba ana majereha kwenye mkono wake. 

Mwanasheria wa bibi yake Katherine Jackson, ameuambia mtandao wa TMZ kuwa Paris anaendelea vizuri na anatibiwa ipasavyo.
Inadaiwa kuwa Paris ambaye ana kaka yake Prince Michael, 16 na mdogo wake Prince Michael II, 11 amekuwa na majonzi yanayosababishwa na kifo cha baba yake aliyefariki miaka mine iliyopita.

0 maoni:

Post a Comment

Labels