Pages

Monday, July 01, 2013

UVUMI KUHUSU RIHANNA KUWA NA MIMBA YA CRISS BROWN


LISEMWALO lipo, kama halipo lipo njiani laja… Rihanna anavumishwa kuwa na ujauzito wa Chris Brown.
 
Uvumi huo ulioripotiwa na mitandao kibao ya habari ya Marekani, umekuja baada ya supastaa huyo wa muziki wa pop kufuta shoo nne za ziara yake ya Diamond World Tour iliyoanza Machi 8 akilalamika kuwa “mgonjwa”.

Kama kuna ukweli kuhusu uvumi huo, hakutakuwa na mshangao mkubwa kwa mashabiki wake, kwani Desemba mwaka jana alisema kuwa anataka mtoto baada ya kurudiana tena na Chris.
 
Rihanna mwenye miaka 25, alionekana akitoka kwenye jengo la matibabu la Beverly Hills jijini Los Angeles Jumanne iliyopita, na wadadisi wanaamini kuwa ziara yake hiyo kwa daktari haina uhusiano na tatizo la koo linaloelezwa kumuweka nje ya steji.
 
Lakini chanzo cha karibu na mkali huyo anayetamba na kibao chake ‘Diamond’ kimesema kuwa hatarajii kupata mtoto.
 
Mtu mwingine wa ndani ameuambia mtandao wa HollywoodLife.com kwamba Rihanna “ni mgonjwa tu”, na akaongeza, “sorry, si wakati huu. Yeye si mjamzito!”

0 maoni:

Post a Comment

Labels