Pages

Monday, July 22, 2013

Rihanna adondosha machozi jukwaani kwa ajili ya fans wake


Robyn Rihanna Fenty a.k.a Rihanna ingawa alikutana na wakati mgumu kwa fans wake kwa kuzomewa na kumwagiwa chakula kwa kuchelewa jukwaani, ameonesha tofauti alipokuwa Lille, Ufaransa kwa kudondodosha machozi kwa ajili fans wake walio-show love ya kutosha jumamosi July 20.

Diamonds hit maker alianza kuongea kwa hisia kuwashukuru fans wake kwa kumuonesha mapenzi tele huku akionesha kuumia kwa kuwa anaelekea kumaliza ‘Diamond Tour’ huko Ulaya, machozi yalimtoka akiwa katikati ya maelezo wakati huo fans hao walizidi kumshangilia.

“Nawapenda wote, asanteni sana. Siwezi kuamini hiki …. Wote mnanifanya nifurahi sana, hiki ni kila kitu chenye maana kwangu, na nasimama hapa na nahisi upendo katika chumba hiki katika ziara yangu hii yote..inaelekea mwishoni na inasikitisha. Nachukia kusema ‘goodbye’. You guys showe me so much love in this room tonight.” Alisema RiRi.

Bada ya maelezo hayo yalitoka moyoni aliendelea kumwaga machozi ya furaha kama ya ‘K-Lyn kwa Bushoke’.

"I don't know why the f**k, I'm crying, that's crazy, thank you so much. I love you guys its a Diamonds World tour so you know we can't leave yet,"alifunguka kisha kuwapigisha shangwe zaidi mashabiki hao kwa kuanza kuiimba hit yake “Diamonds”.

Baada ya performance shabiki mmoja alipost picha ya Rihanna na kuiweka Instagram na kuandika “You saw me crying and you started to cry. So much emotions for the last show. I miss you so much I love you.”

Rihanna alijibu ujumbe huo, “it's all your fault! LOLOLOLOLOLOL! I felt you! You help me to understand how a fan really thinks! The way you guys appreciate it all, it kills me I can't believe how much you guys really love me! You care so much, its overwhelming and yet so beautiful!”

hakuishia hapo akaendelea kubonyeza button na kuandika “Thank you is all I can say! Thank you Thank you Thank you all! My fans are truly my gift from God! And I thank him everyday for it!”

RiRi anatarajia kumaliza tour yake ulaya July 28 nchini Finland kisha atatembelea Asia, Australia na Afrika..na kukamilisha mzunguko huo kwa kuihamishia Marekani mwezi November mwaka huu.

0 maoni:

Post a Comment

Labels