Kutokana na sababu ambazo hazijatajwa, kampuni hii yatangaza 'bifu' kali na Chris Brown
Moja wa wadhamini wa
show kubwa kabisa ambayo ita-happen huko Canada mwezi ujao, wamejitoa
katika mpango huo mara baada ya kugundua kuwa Msanii Chris Brown
ameongezewa katika listi ya wasanii watakaoperform.
Kampuni
hii maarufu ya Rogers Communication haijatoa sababu yoyote ya ndani
kuhusiana na ni kwanini wamejiondoa katika udhamini wa tamasha hili ila
kwa mujibu wa moja ya wasemaji wa kampuni hii, uamuzi wao ni kutokana na
msimamo waliojiwekea kuwa, hawatajihusisha na wala hawataki kujihusisha
na shughuli yoyote ambayo kwa namna moja ama nyingine inamhusisha Chris
Brown.
Onyesho hili litafanyika huko Canada Halifax August 31 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment