Pages

Monday, July 22, 2013

RAPPER KANYE WEST AMTEMBEZEA KICHAPO PAPARAZI

Kanye West this tym round ameamua kufanya kweli kwa kumpatia kichapo Paparazzi ambaye aliingia kwenye kumi na nane zake vibaya katika kipindi hiki ambacho rapa huyu amekuwa mkali kupita kiasi na kuonyeshwa kukerwa na tabia za wanahabari hawa kumfuatilia kupita kiasi.

Tukio hili ambalo lilinaswa vizuri kwenye picha na wanahabari wengine limetokea huko Los Angeles mchana kweupe siku ya jana ambapo rapa huyu kama kawaida alitoa onyo kali kwa mapaparazi waliokuwa wakimfuatilia akikataa wasiongee na yeye.Katika tukio la kushangaza, rapa huyu baada ya kuishiwa uvumilivu alimwambia moja ya ma-Paparazzi hao kuwa wanachokifanya ni sawa na kujaribu kumuingiza katika matatizo awalipe fidia, na kabla somo hili halijaeleweka poa, Kanye alimdaka mnyonge wake na 'kumminya' vilivyo huku akitaka kumnyanganya camera yake, wakati huo mapaparazzi wenzake wakifurahia kuchukua picha za tukio hilo.
Inaelezwa kuwa, Polisi walifika eneo la tukio mara baada ya Kanye kuondoka na walilazimika kumuwahisha mshkaji aliyepewa kisago Hospitali na mpaka sasa duru zinaendelea kufuatilia mwisho wa tukio hili utakuwaje. 
 
Mshkaji huyu aliyeshabuliwa na Kanye ambaye amefahamika kwa jina Deno, alikwishawahi kushambuliwa na Britney Spears pia mwaka 2007 na kupewa kichapo na mwamvuli, na kufutia tukio hili la jana, kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, mshkaji huyu amedhamiria kumfungulia Kanye shtaka la jaribio la kumwibia.... :).

0 maoni:

Post a Comment

Labels