Wananchi,wasomaji pamoja na wauzaji wa rejareja wa
jarida la Rollingstone, wameshangazwa na kuchukizwa na hata kufikia kusema kuwa
ni sawa na kutusiwa na cover jipya la jarida hilo linalotarajiwa kutoka mwezi
wa nane, ambalo limepambwa na sura ya kijana aliesababisha mauaji ya Boston
Marathon, "Dzhokhar Tsarnaev"
cover hiyo yenye picha nzuuri ya mtuhumiwa huyo
ilikuwa na maneno haya.
"THE BOMBER, "How a
popular, promising student was failed by his family, fell into radical Islam
and became a monster.
malalamiko ya kitendo cha jarida hilo kumpamba muuaji huyo wa mabomu ya boston ambayo yaliua watu watatu, kujeruhi
zaidi ya 200 pamoja na ofisa wa polisi mmoja, yalianza kusambaa kupitia
mitandao ya kijamii, facebook pamoja na twitter.
Baada ya malalamiko hayo kuenea, maduka maarufu
yanayouza majarida hayo yametangaza kugoma kuuza jarida hilo, duka la
madawa nchini marekani CVS limetangaza mgomo wa kutokuweka jarida hilo
kwa ajili ya kuuza na kuungwa mkono na makampuni mengine makubwa kama Walgreens,
duka la glosaries lililopo New England "Stop and Shop", pamoja na
Tadesch food shop
kikubwa kinacholalamikiwa ni cover hiyo kuwa na
picha ya muuaji wa mabomu, na picha kumuonyesha kama ni innocent na kudai kuwa
hakustahili kuwa kwenye cover ya jarida hilo.
licha ya malalaniko hayo, wako waliounga mkono
gazeti hilo na kusema kuwa, picha haimaanishi itamfanya muuaji awe ni mtu
mzuri, bali kilichoandikwa, na kilichaandikwa na RollingStone ni maisha
aliyokuwa akiishi kijana huyo na kilichompelekea mpaka kuwa monster, kitu
ambacho ni kizuri kwa watu kuelewa na ni kazi kubwa iliyofanywa na jarida hilo
kupata information zote hizo.
0 maoni:
Post a Comment