Produza Lamar akiwa kwenye studio zake Fishcrab
Lamar kutoka studio zake za Fish Crab amesema kuwa hivi sasa anasaka
wasanii wanaume wenye vipaji vya kuimba kwa kiingereza na kiswahili.
Lamar alisema kuwa anafanya hivyo kwakuwa mwaka uliopita alifanya
mchakato huo huo wakutafuta vipaji kwa upande wa wasichana ambako
alifanikiwa nakupata wasichana watatu ambao hivi sasa ndo wanaunda kundi
la wasanii wa kike 'Shosteez'.Kwa sasa anasema anataka kutengeneza
kundi la wasanii wa kiume wanaoimba kama alivyofanya kwa wasanii wa
kike.
Lamar akiwa na kundi ambalo analisimamia hivi sasa 'Shosteez'
Kama wewe ni kijana wa kiume una uwezo nenda katika studio za Fishcrab
zilizopo maeneo ya Kariakoo au unaweza kutuma 'demo' yako ukiwa
unaimba kupitia anuani ya barua pepe ambayo ni fishcrab@gmail.com, alisema Lamar.
0 maoni:
Post a Comment