Pages

Thursday, April 18, 2013

[VIDEO]:-NEY WAMITEGO FT DIAMOND NA MUZIKI GANI
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Elibariki Munishi ‘Ney wa Mitego’ ameanza kurekodi video ya wimbo wake, ‘Muziki Gani’ aliomshirikisha Nassib Abdul ‘Diamond’.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Ney alisema kwamba video hiyo inayotarajiwa kuwa ya aina yake, itarekodiwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kazi ya kutayarisha video hiyo imefanywa na Kampuni ya Visual Lab chini ya Adam Juma, hivyo amewataka mashabiki kukaa tayari kuipokea kazi hiyo pindi itakapokamilika.

Ney ambaye amekuwa akitoa nyimbo zinazomletea msigano na wasanii wenzake, aliongeza kwamba pamoja na ‘singo’ yake hiyo kuendelea kutamba, anaendelea na mpango wa kutayarisha kazi mpya.

“Nawashukuru mashabiki wangu kwa kuzipokea vizuri kazi zangu, sina cha kuwalipa zaidi ya kuendelea kuwapa kazi nzuri zaidi,” alisema.

Baadhi ya nyimbo alizopata kutoka nazo msanii huyo ni pamoja na ‘Nasema Nao’, ‘Wamenichokoza’, ‘Ndolela’, ‘Itafahamika’ na nyinginezo.

1 maoni:

Post a Comment

Labels