Pages

Tuesday, April 30, 2013

Barua ya wazi kutoka kwa mdau wa BONGO FLEVA.

Naitwa Mtanzania Halisi Machungu !

Ninao ujumbe mdogo kwa jamii ya burudani hapa nchini,wiki iliyopita Tuzo za muziki wa Tanzania zilitangaza majina ya wahusika watakuamo kwenye kinyang’anyiro hicho kwa mwaka 2013 ni sawa kabisa wala sina la kuhoji kwa kuwa tayariwametajwa hao pekee.

Point yangu hapa ni kwa baadhi ya categories, kuna nyimbo kama sorry ya barnaba boy ni ya mwaka huu kabisa lakini imo na inawania tuzo,sasa basi waache ubabaishaji kabisa na pia kuna category ni THT tupu hii ina maana kuwa tuzo imeenda THT hakuna nafasi kwa watu wengine hiyo si kweli.

Sina maswali sana na categories nyingine, hip hop hivi fid q hua hajui au ni kwa nini hapewagi award na kwa nini hathaminiwi na kura watu hua tunampigia sana tu,hata hao watoto watamdharau mwisho wa siku wakati hawana hata robo ya uwezo wake.

Kwenye raga naomba watanzania wenzangu tufunguke macho na tuachane na uongo unaopangwa kuna jamaa anaitwa dabo huyu jamaa siamini kama kuna hata mmoja kati ya waliopangwa nae wanaomuweza baada ya raia kupiga kura sijui hua kuna nini kinafuata mpaka hapewi tuzo mwaka huu naomba haki itendeke na jamaa apewe tuzo yake wasisubiri afe.

Dada yetu Jide nakubali ni legendary lakini kwa mwaka jana hakua na heat yoyote labda wanamuogopa tu kwa kweli kwa utajiri wake,halafu kwa upande mwingine kuna dogo anaitwa belle 9 nae wanamnyanyasa sana kiukweli hali itendeke hapa sio kilasiku diamond au dimpoz ni ujinga.

Mambo ni hayo tu kwako Mtanzania mwenzangu unaetaka maendeleo ya muziki wetu lazima ukweli uonekane.Ni hayo tu !!!!!

0 maoni:

Post a Comment

Labels