Huu ndio usafiri wa msanii Lackson aliokuja nao leo
Huyu ndie msanii Lackson aliyetuhumiwa kumloga mwenzake leo afichua siri ya kutuhumiwa
Huyu ndie msanii Magumash akiwa katika gari ya mhasimu wake aliyedai awali kuwa analoga kazi zake zisipate soko
Msanii maarufu wa Filam mkoa wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi kulia akiwa na msanii Lackson ambae alimtuhumu kuwa ni mcahwi
hapa wasanii hao wakionyesha umoja baada ya kumaliza tofauti zao na kuwa kitu kimoja
LILE sakata la msanii maarufu wa Filam mkoa wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi kudai kulongwa na msanii mwenzake Lackson Luwema limemalizika baada ya mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwakutanisha mahasimu hao na kumaliza tofauti yake huku Lackson akitoa siri ya kuzushiwa mambo kuwa ni kutokana na jitihada zake.
Msanii Luwema ambae ni mmoja kati ya manguli wa kuigiza Filam mkoani Iringa amesema kuwa kwa upande wake katika mkoa wa Iringa amekuwa akifanya vema katika tasnia ya filam na kuwa hakuna msanii wa mkoa wa Iringa ambae hajui jitihada zake.
Luwema alisema kuwa mbali ya kuonyesha uwezo katika tasnia hiyo ya uigizaji ila bado yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanafanya kazi kwa kumtegemea mwenyezi Mungu zaidi kwani yeye amekulia katika mazingira ya ulokole hivyo kamwe hatajiingiza katika mambo ya shetani ya kutumia ndumba katika kazi hiyo ambayo anaamini ni kipaji toka kwa mwenyezi Mungu.
Hata hivyo amesema kuwa tatizo la wasanii wengi wa mkoa wa Iringa hawataki kujibidiisha kwa kuboresha kazi zao na badala yake wamekuwa wakikurupuka katika kuingia katika tasnia hiyo bila kujiandaa vya kutosha na mara baada ya mambo kwenda kombo ndipo huanza kutafuta mchawi wa kukamwa kwao huku wakitambua kuwa wameingia kichwakichwa katika fani.
Msanii Luwema ameendelea kujizolea umaarufu mkubwa kupitia filam zake mbali mbali ambazo amepata kutoa ikiwemo la Polisi Jamii,Yoshua na Stress na sasa ni mmiliki wa kundi la sanaa la Mundu sanaa Group ambalo limeendelea kutikisa vichwa vya wasanii mkoani Iringa .
Akieleza malengo yake ya mbele amesema kuwa kwa sasa yupo mbioni kutoka filam nyingine inayokwenda kwa jina la Hostages ambayo itakuwa ni funika mbaya na kuwataka watanzania kujiandaa kuona filam hiyo.
Kwa upande wake msanii Magumashi baada ya kukutanishwa pamoja na kuelezwa ukweli na msanii huyo aliyekuwa akihisi kuwa kikwazo cha maendeleo yake ameupokea ushauri uliotolewa kwake na kuafikiana kumaliza tofauti zao na kuchapa kazi zaidi.
HII NDIO STORI YA AWALI ILIYOCHAPISHWA HAPA JUNE 25 ,2013
MSANII FILAM IRINGA ADAI KULONGWA NA MSANII MWENZAKE
Msanii maarufu wa Filam mkoa wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi akionyesha kazi zake
MBALI ya kupiga hatua katika tasnia ya
uigizaji na kufanikiwa kutoa DVD inayokwenda kwa jina la Bi MUWASHO
ambayo imetokea kupendwa zaidi na watanzania ambao wamefanikiwa
kuinunua ,msanii maarufu katika uigizaji mkoa wa Iringa Erasto Kilowoko
a.k.a Magumashi ametinga ofisi za mtandao huu wa www.matukiodaima.com na kuibua tuhuma dhito dhidi ya msanii mwenzake kuwa amekuwa akiloga kazi zake.
Msanii huyo alisema kuwa msanii
ambae amekuwa akimloga ni kiongozi wa wa kundi la sanaa mjini
Iringa ( jina lake limehifadhiwa ) na sababu za kufanya hivyo ni
kutokana na kuona mafanikio makubwa ambayo ameanza kuyapata na
kufanikiwa kulitupa mbali kundi linaloongozwa na msanii huyo mwenye
roho ya kwanini.
Magumashi amesema kuwa kazi ambayo
ameitoa inayokwenda kwa jina la Bi Muwasho ameisambaza katika mkoa
wa Ruvuma, Dodoma na Iringa na kuwa kazi hiyo imepokelewa vizuri
na wadau wa sanaa ya maigizo na hivyo kupelekea kiongozi huyo wa
kundi la Sanaa linalofanya mazoezi yake katikati ya mji wa Iringa
kuingiwa na hofu na hivyo kuanza kutumia ndumba kuzoofisha jitihada
hizo.
Hata hivyo mbali ya kumuonya
kiongozi huyo Mlogi bado amesema yeye anamtegemea zaidi Mwenyezi Mungu
na kuwa kamwe jitihada zake za kukwamisha kazi zake hazitafanikiwa
kwa sasa.
Pia alisema kwa sasa yupo mbioni kutoa kazi nyingine inayokwenda kwa jila la Kiboko yao ambayo itakuwa funika mbaya .
Akielezea kwa masikitiko makubwa juu ya
ubaya anaofanyiwa na kiongozi huyo wa kundi la sanaa mjini Iringa
amesema kuwa hivi sasa mbali ya kutoa kazi ya kwanza na kuendelea
kuiandaa ya pili ila bado hakuna maendeleo yoyote na pesa anayoipata
hafanyii kituo chochote cha maendeleo na hadi sasa hana pesa hata
ya kununua kiatu wala kandambili
CHANZO:-http://www.matukiodaima.com
0 maoni:
Post a Comment