Msanii
anayekuja kwa kasi katika muziki wa Bongo Flava hapa nchini Tanzania,
ambae pia amaeshafanya colabo na wasanii wakali katika gemu akiwemo
Linex, Suma Mnazareth, Nick Maujanja na wengineo muite Wynem jina halisi
anaitwa Mahamud Issa.
Gemu la muziki wa kizazi kipya alianza mwaka 2000
wakati akiwa anasoma kidato cha nne huko Mkoani Morogoro, wakati akiwa
shule hakutaka kuchanganya muziki na masomo mpaka pale alipomaliza ndipo
akaingia rasmi kwenye muziki.
Alipomaliza chuo 2007 akaanza kazi huku
akifanya muziki lakini muda mwingi alikuwa kwenye kazi ikawa ngumu sana
kufanya muziki.
Mwaka 2009 alishirikishwa na Nick Maujanja kwenye ngoma
inaitwa “SMS” ngoma ambayo ilifanya fresh sana Channel O ikiwa kwenye
chart kwa wiki tatu mfulululizo katika Viewers Edition.
Pia
alishashirikishwa na Suma Mnazareth kwenye ngoma ya “Tofauti na jana”
baada ya hapo akashirikishwa kwenye ngoma ya Linex inayoitwa “Maumivu” .
Baadae akafanya ngoma kwa ajili ya jamii inayoitwa “Japo Kidogo” .
Akarudi Chuo akawa amepumzika kufanya muziki. Sasa amerudi na ngoma
inaitwa “Mwanambuzi” iliyofanywa ndani ya studo za GZ Records.
Mshikaji
anapostigraduate diploma ya kodi aliyoisoma katika chuo cha kodi
mikocheni Dar es salaam.
0 maoni:
Post a Comment