Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, June 30, 2013

List ya ngoma zitakazo patikana ndani ya Magna Carta Holy Grail...

Jay-Z, Justin Timberlake, Nas and Timbaland in-studio together
Baada ya Jigga kutangaza kutoa Albam mpya Julai 4 Mwaka huu sasa List ya track zitakazo patikana ndani ya hiyo albam tayari imesambaa kupitia mitandao na mimi kuidaka.
1. Picasso Baby
2. Heaven
3. Versus
4. Tom Ford
5. Beach Is Better
6. FuckWithMeYouKnowIGotIt
7. Oceans
8. F.U.T.W.
9. Part II (On The Run)
10. BBC
11. La Familia
12. Jay-Z Blue
13. Nickles & Dime
s

BAADA YA KUTOKA JELA JA RULE KUACHIA BONGE LA MOVIE OKTOBA MWAKA HUU


Ja Rule hivi sasa anapromote movie yake mpya 'I'm In Love With a Church Girl',alioifanya na mtoto mzuri  Adrienne Bailon.

Ndani ya hiyo movie Rule amecheza kama jamaa alieamua kuachana na uuzaji wa dawa za kulevya yaani former drug dealer ambaye amechoshwa na maisha aliyoyapitia na ku fall in love kwa msichana wa kanisani kutoka kwenye familia ya dini.

Mausiano yao yanakuwa katika wakati mgumu ja rule anapoteza marafiki na anawindwa kutokana na matukio yake ya mtaani aliyoyapitia pia inawawia vigumu kujenga mahusiano yao .
movie hiyo inatarajia kutoka October 18 Mwaka Huu.

'' IMANI YANGU HAINIRUHUSU KUTANGAZA NINAPOTOA MISAADA''Mwana FA.


MSANII maarufu wa Hiphop nchini, Khamis Mwinjuma au maarufu Mwana FA,amesema muziki kwake ni kazi na sababu inayomfanya kila siku azidi kung’ara ni ubunifu alionao ambao humfanya kuwa tofauti na wenzake.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii alisema,muziki ni kazi hivyo inabidi kila siku kufikiria vitu mbalimbali ambavyo atawaletea mashabiki wako ili wazidi kumpenda na kumfanya kutochuja katika muziki”muziki ni kazi hivyo mara nyingi nimekuwa najaribu kubuni aina mbalimbali zaa maneno ili niwe tofauti,kama Unanitega,Bado niponipo na mengine mengi tu,ilio tu yawe mapya kwa mashabiki”.

Akielezea historia yake alisema,muziki alianza toka mwaka 1993 ambapo alifanikiwa kuanzisha kundi ambalo lilikuwa linaitwa,Crew Black Skin na katika kundi hilo alikuwa na marafiki zake wawili ambao ni Robilus na Getheerics.

Mwana FA alikutana na marafiki zake hao kipindi wakiwa katika shule ya Umumio Islami High School,kwani wote kwa pamoja walikua wanachukua masomo ya Sience.

Mnamo mwaka 2000 alifanikiwa kutoa nyimbo yake ya kwanza iitwayo”Ingekuwa vipi”ambayo alimshirikisha Juma Mchopanga”Jay Moe”ambayo ilifanikiwa kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa.

Baada ya nyimbo hiyo alifanikiwa kutoa nyingine kama “Mi na mabinti””Show time”,aliyomshirikisha Ambwene Yessaya”AY,Alikufa kwa ngoma,ambayo alikuwa amemshirikisha Judith Wambura”Lady jay Dee”.
Mwana falsafa kwa mara ya kwanza alifanikiwa kupata tuzo ya Kilimanjaro Music Awards mwaka 2003 kupitia wimbo wake wa,Alikufa kwa ngoma,ambao ulichaguliwa kuwa wimbo bora.

Baada ya kupata tuzo hiyo alitoa albamu ya kwanza iitwayo Mwanafalsafani,ambayo alisema ilifanikiwa kufanya vizuri na hivyo kupata hamasa ya kuendelea kufanya Albamu nyingine ambapo mwaka uliofuata mwishoni alitoa Albamu ya Unanitega,ambayo pia mwaka 2006 ilimpatia tuzo ya Albamu bora ya Hiphop.

Mnamo mwaka 2007 pia mwana FA akiwa ameshirikiana vizuri na AY,walifanikiwa kupata tuzo kupitia wimbo wao wa “Habari ndio hiyo”kuchaguliwa kuwa wimbo bora wa mwaka”nilifurahi sana baada ya kupata tuzo,kwani naamini kila kazi mwisho huwa na mshahara,tuzo ni heshima na ilinipa hamasa kwa kiasi kikubwa sana ya kuzidi kuongeza juhudi katika fani hii na kuzidi kuwa mbunifu”.

Mwana FA ambaye alizaliwa mwaka 1984,kwa kushirikianna na rafiki yake wa karibu,Ambwene Yessaya walifanikiwa kutoa Albamu moja iitwayo”Habari ndio hiyo”,ambayo ndani yake kulikuwa na nyimbo kama“Kula kwa macho”waliyomshirikisha msanii kutoka nchini Uganga”Talia”,”Asubuhi”ambayo walimshirikisha Abubakar Katwila “Q chief”,”Fungua champagne”,”Nangoja ageuke”,”Bounce”,na “Umejuaje”.

Mwana FA hadi sasa tayari ana albamu nne ambazo tayari ameshazitoa,ila kwa sasa amesema albamu hazina faida hivyo yeye atakuwa anatoa nyimbo tu na kufanya maonyesho,kwani anaamini kipato kikubwa kipo katika maonyesho”Kwa sasa sina mpango wa kutoa Albamu kwa sababu unajua hailipi,tumekuwa tunaibiwa sana kiasi kwamba mtu unafanya kazi kubwa ila mwisho wa siku faida haionekani”Albamu hizo ni Mwanafalsafani,Toleo lijalo,Unanitega,Habari ndio hiyo.

Akizungumzia mafanikio ambayo ameyapata hadi sasa anasema ni makubwa sana kiasi kwamba hana budi kumshukuru sana mungu kwa alipofikia kwani hakutaraji kama atafika ila pia bado anazidi kumuomba mungu,kila siku azidi kumpandisha juu zaidi ya hapo”Namshukuru sana mungu na wazazi wangu ambao wamenilea ila kwa kweli nawapongeza na kuwashukuru pia mashabiki kwa kuwa bila wao mimi nisingekuwa hapa nilipo”

Akizungumzia kuhusu watu wachache ambao wamekuwa wakihusisha mafanikio yake na kundi la FreemaSon,alisema umefika muda sasa wa Tanzania kuamka na si kwamba kila mtu anayefanikiwa ni kumhusisha na kundi hilo ”nawaomba wa Tanzania wenzangu wabadilike,si kwamba kila mtu anayefanikiwa basi ameingia katika kundi hilo,mimi ni msanii wa zamani sana hivyo mafanikio nastahili,pia ukizingatia kuwa ni msanii ambaye ninakubalika katika jamii”.

Mwana FA alipoulizwa kuwa anaisaidia vipi jamii inayomzunguka hasa wajane na wale watoto wenye ulemavu alisema,huwa anasaidia kupitia mfuko wa Sawasawa Foundation,ambapo hupeleka misaada yake kwa ajili ya kusaidia watoto yatima na wajane”Unajua imani ya dini yangu huwa hainuruhusu kutangaza pale ninapotoa msaada,sababu hiyo ndio maana huwa nakuwa kimya tu,ila nasaidia kupitia mfuko wa Sawasawa Foundation”
“Na malengo makubwa sana,hasa mwaka huu,kwani nimejipanga vya kutosha kuhakikisha nitafanya mambo makubwa kuliko mwanzo,amini nimejipanga vya kutosha ili nizidi kuwa juu zaidi”
 

LIST YA TOP 20 | KITULO FM | TOP TWENTY 30 JUNI 2013


Nafasi Wiki Hili
Jina la Wimbo na Msanii
Nafasi Wiki Lililopita | Ingizo Jipya.
20
Res Of Ma Life – Hemedy f| Mr Blue
Ingizo Jipya
19
Jikubali – Ben Pol
20
18
Let me know - Chin  Bees  f| Nah Real & Haika 
Ingizo Jipya
17
Sio Mimi – Madee f| Raymond
17 For 2 weeks
16
No Beef – Ngwea f| T.I.D
16 For 2 weeks
15
Muziki Gani – Ney wamitego f| Diamond
15 For 2 weeks
14
Ukimuona – Diamond
08
13
Joto,Hasira – Lady Jaydee f| Prof J
11
12
Jipe Shavu – A.Y f| Fid Q
14
11
Sina Imani – Setta f| Rich Mavoko
04
10
Masebene – Y-Tony
10 For 2 weeks
09
Furaha ya Leo – Dream
13
08
Attention – M-Rap f| Deddy
12
07
Love Me – Izzo B f| Barnaba & Shaa
07 For 2 weeks
06
Wanipa wazimu – Lawize Entertainer f| Ney Lee [Super Nyota]
06 For 2 weeks
05
Riziki yangu – Linex f| Wayre
09
04
Jitunze – Mr R.E.D
05
03
Uzuri wako - Jux
03 For 2 weeks
02
Sina Makosa - Timbulo
02 For 2 weeks
Wimbo wa Ziada
MWALI KIGEO - RACHEL

01
Maisha ya Skonga – Janjaro f| PNC
01 For 2 weeks



LIST YA NYIMBO 20 IMEANDALIWA NA MUSIC DEPARTMENT YA KITULO FM

01:-DJ NUNDU | PAMOJA NA

02:-ERGON ELY The Pitch Controler



Production Imesimamiwa na:-

Ergon Elly The Pitch Controler



KWA MAONI | USHAURI | PENDEKEZO |KURA TUTUMIE KUPITIA

Email:-ergonsanga@yahoo.com au kitulofm@yahoo.com

Simu:-0718 742 990

Tunakutakia  Jumapili NJema!!!

CRISS BROWN | CHRIS BROWN AMKANA MISS URUSI NA KUMWITA MALAYA

Mwanamuziki wa Pop Chris Brown ameanzisha vita vya maneno na Miss Urusi baada ya kumwita mwanamke huyo malaya.

Brown hivi karibuni aliripotiwa kuwa na mahusiani ya kimapenzi na Olga Gure Kovalenko ambaye ni Miss Urusi 2013, lakini msanii huyo aliibuka na kudai kuwa hakuwa na haja na binti huyo zaidi ya kumchukulia kama malaya na alimtaka kwa ajili ya kufanya naye mapenzi na kumwacha.

PICHA | UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA BAGHDAD F| NEY WAMITEGO & CHID BENZ - WAAMBIE NIPO

Nay wa Mitego akifanya mambo yake katika hiyo Video
Chidi Benz akiwa na warembo
Baghdad akiwa na Chid Benz na warembo walio jitokeza

CPWAA NA SUMALEE WAIREJESHA UPYA PARKLANE

Kundi la Parklane lililokuwa likiundwa na Sumalee na Cpwaa linarudi tena baada ya wasanii hao kuachana kwa muda na kila mmoja kuendelea na solo projects kwa mafanikio.

Taarifa hiyo imetolewa wiki hii na Cpwaa ambaye jina lake ni Ilunga Khalifa kwenye kipindi cha The Jump Off cha Times FM.

Yeyote ambaye anasikiliza sasa hivi, ajue kwamba Parklane tayari imesharudi na tumeshaingia studio na tumeshagonga ngoma karibia mbili na moja wapo itatoka kabla ya mwezi wa Ramadhan, kwahiyo Parklane imerudi na watu wakae tayari kwa ujio mpya wa Parklane, Sumalee na C to the Pwaa,”alisema Cpwaa.

Kundi la Parklane liliwahi kutamba na nyimbo kadhaa ukiwemo Nafasi Nyingine uliorekodiwa kwenye studio za Tabasamu Records za Mombas

RICK ROSS ''ROZAY'' AZAMA KWENYE MSALA #ANADAIWA SHILINGI MILIONI 145

Rick Ross The Boss mwenyewe wa MMG This Time round kwenye headlines na hii hapa tena.... story ni kwamba rapa huyu kwa sasa anakabiliwa na mashtaka/madai ya fidia kutokana na kutokulipa deni alilokuwa nalo baada ya kununua saa tatu za dhahabu aina ya Rolex zenye thamani ya dola  $89,847.50, ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 145 za kitanzania.

Kutoka huko Texas Marekani, Johnny's Custom Jewelry ndio wadai wa msanii huyu, na madai yao ni dhidi ya Ross na May bach Music Group kwa ujumla, ambapo bishara hii ambayo mwisho wa siku haikukamilika ilifanyika mwezi August mwaka jana.

Taarifa za kiuchunguzi zinasema kuwa, kwa muda wote huo Johnny's Custom Jewelry wamekuwa wakimsikilizia Ross kulipa 'mulla' yao kistaarabu kutokana na hadhi yake, lakini kutokana na muelekeo wa mambo, kwao imeonekana dhahiri kuwa hakuna dalili yoyote ya malipo na muda ndio unazidi kuyoyoma.

Friday, June 28, 2013

NEY WA MITEGO Na DIAMOND PLATNUMZ Kuachia Ngoma Nyingine Mpya



Wakali wa ngoma “MUZIKI GANI” , yaani Nay Wa Mitego Na Diamond wako njiani kuachia ngoma nyingine wakiwa katika collabo … Inasadikika kuwa Platnumz na Wa Mitego wamesharekodi ngoma kadhaa ikiwemo SALAMU ZAO, UTAKULA JEURI YAKO na nyinginezo ila wanashauriana ni ipi ya kutoa.

MUZIKI GANI imefanya vizuri sana na wasanii hawa na hakutakuwa na tatizo kama wakiendeleza kazi zao kwa pamoja.

Wasanii hawa wako kwenye ziara zao tofauti kimuziki lakini tuwategemee tena na ngoma nyingine kali.

TOP 10 | NYIMBO KUMI ZA WIKI 28 JUNI 2013 AT KITULO FM


Namba
         Jina la Wimbo na Msanii
10
Wasi wasi - Vumbe
09
Muziki Gani – Ney wamitego F| Diamond
08
Riziki
yangu – Linex F| Wayre
07
Jipe Shavu – AY F| Fid Q
06
Wanipa wazimu – Lawize Entertainer F| Ney Lee [Super Nyota]
05
Jitunze – Mr R.E.D
04
Jikubali – Ben Pol
03
Uzuri wako - Jux
02
Sina Makosa - Timbulo
01
Maisha ya Skonga – Janjaro F|  PNC


NEW HIT SONG | JOH MAKINI F| FUNDI SAMWEL NIKUMBATIE

Thursday, June 27, 2013

Hukumu Ya Fat Joe Kwenye Kesi Ya Kukwepa Kodi Imetajwa.

December mwaka jana Fat Joe aka Joseph Cartagena alikubali kosa la kukwepa koda zilizo takiwa kulipwa katikati ya mwaka 2007 na 2008, na alikuwa akisuburi hukumu. Fat Joe alitengeneza dola milioni 3 kwenye muda huo na kwamba hakulipa koda mpaka mwaka 2010. Well walisema angepatikana na hatia, adhabu ilikuwa miaka 2 ila jana amehukumiwa miezi minne jela, na faini ya dola $15,000 fine, Fat Joe ataanza kutumikia kifungo chake August 26 2013.

Muingiliano wa majina ya bidhaa zao ndio chanzo cha ugomvi ambao unawakabili mastaa hawa kwa sasa.

Imefahamika kuwa, Msanii wa muziki Will.i.am ameamua kumfungulia mashtaka msanii na mtayarishaji muziki Pharell Williams kwa kesi ya madai kutokana na hatua ya Pharel kutumia jina la I AM OTHER katika bidhaa zake mbalimbali anazozalisha zikiwemo Mavazi.



Will.i.am amesema kuwa, jina hili na logo vinakaribiana/vinashabihiana/vinafanana kwa karibu nha brand yake ya WILL.I.AM, na msanii huyu amenuia kutumia sheria kumzuia Pharrel kufnya biashara kwa jina I AM OTHER katika bidhaa zake.

Hii ndiyo Brand mali ya Pharell ambayo Will.i.am hakubaliani nayo.

Tayari wanasheria wa Pharell wamekwishajibu mashambulizi kwa kujibu mashtaka haya kwa maandishi kuwa madai ya Wil.i.am hayana msingi wowote.

Rekodi ya Chris Brown kupishana maelewano na vyombo vya dola inaendelea kuchafuka, Huu hapa ni msala mwingine ambao unamkabili kwa sasa.

Chris Brown, muda mfupi tu akiwa anakabiliana na tuhuma za kumdhalilisha mtu katika moja ya kumbi za starehe mwishoni mwa wiki, sasa mapya yamemuibukia msanii huyu ambapo sasa imefahamika kuwa amefunguliwa mashtaka ya kusababisha ajali na kukimbia.


Hii ni kutoka tukio la mwezi uliopita ambapo msanii huyu aliripotiwa kusababisha ajali ndogo ya gari dhidi ya mwanamke ambaye kwa mujibu wa mashtaka, staa huyu alikataa kumpatia taarifa sahihi za leseni na bima yake.

Tayari Chris Brown ameshajibu tuhuma hizi kwa njia ya mtandao na kusema kuwa, mwanamke huyu alikuwa anatafuta namnaya kukuza mambo kwa sababu baada ya kumgonga, alisimama na kuelewana naye, isipokuwa mwanamke huyu alikuwa na nia ya kukuza mambo baada ya kugundua kuwa ana-deal na staa mkubwa katika tukio hili.
Msanii huyu amesema kuwa kwa sasa tayari wanasheria wake wanalishughulikia swala hili ambalo ameliita uzushi mkubwa kutokana na gari la kwake na la mwanamke aliyemgonga kutopata madhara yoyote, na pia kutokana na msanii huyu kuonyesha kujali kuchukua muda wake na kuzungumza na adui yake.

Kupitia ushahidi huu, Prince Jackson, Mtoto wa Michael Jackson aamsha upya hisia za watu kuhusiana na Daktari Conrad Murray ambaye anatumikia kifungo kwa sasa kutokana na kifo cha Michael Jackson.

Mtoto wa Michael Jackson, Prince jackson naye amepanda kizimbani kutoa ushahidi wake katika kesi mpya inayoendelea sasa ya Kifo cha Michael dhidi ya kampuni ya AEG Live ambayo ndiyo ilikuwa inaandaa onyesho lake la mwisho, ambapo ushahidi wake umemlenga tena Dr. Conrad Murray na kugusa hisia za wengi pale mtoto huyu alipoelezea namna daktari huyu alivyowafikishia habari za kifo cha baba yao

Paris na Prince Jackson - Watoto wa Michael Jackson

Prince Jackson amesema kuwa, anakumbuka siku ya kifo cha baba yake, alikuwa ameketi sebuleni katika jumba lao la Hombly Hills wakati ambapo baba yao alizidiwa, na ndipo alipoanza kusikia kelele, na Daktari huyu alimwita chumbani alipokuwa Michael wakati akijaribu kumfanyia huduma za mwisho na mwisho wa siku katika hali ya kutokujali, Daktari huyu aliwaeleza moja kwa moja kuwa baba yao tayari amekufa ['Sorry Kids. Dad's Dead.'].
Dr Conrad Murray
Maelezo haya yamegusa kwa kiasi kikubwa hisia za Daktari huyu (Conrad Murray) ambaye mpaka sasa anatumikia kifungo kwa makosa ya kusababisha kifo cha Michael.

Prince pia ameweka wazi ni kwa jinsi gani kifo cha baba yao kilivyomuathiri kwa kiasi kikubwa mdogo wake, Paris ambaye mpaka sasa yupo katika kipindi kigumu kukabiliana na hali halisi.

NEW SONG | MWANA FA & AY F| J.MARTINS - BILA KUKUNJA GOTI

PICHA | 30 JUNI NI USIKU WA NGWEA SAMAKI SAMAKI TRIBUTE


PICHA | OMMY DIMPOZ NA NAI NAI USA TOUR NI AMERICA NA CANADA


Wednesday, June 26, 2013

NEW AUDIO | SPINCE SESEME - ROHO ZINAWAUMA

PICHA | TID LIVE IN DUBLIN ON SATURDAY | 6 JULY 2013


PICHA YA SIKU

Katikati Msanii kutoka katika kundi la muziki Wilayani Makete Y-Jay na Kulia ni Mtangazaji wa Redio Kitulo Fm Ergon Elly

Thursday, June 20, 2013

Lil Wayne Kaboa Mashabiki Zaki Kinoma.

 

Rapper Lil Wayne ameonekana kukosa Heshima kwa nchi yake Baada ya picha za rapper huyo kusamba zinazo muonyesha akikanyaga bendera ya Marekani. Kwenye utengenezwaji wa video ya single yake mpya ya `God Bless Amerika' mafundi wanaonekana wakiweka vizuri bendera hio na baada ya muda Lil Wayne anaonekana anaikanyaga mbele za watu.
Video na picha za kitendo hichi zinaonekana kutoka kwenye simu ya mtu aliyo kuwa eneo la tukio. Mstari wa Lil Wayne unaozungumzia Marekani kwenye huu wimbo Ndio Huu
 “My country ‘tis of thee/ sweet land of kill ‘em all and let ‘em die/ God bless Amerika/ This so godless Amerika … the stars on the flag are never shining.”

Mpenzi wa Balotelli awa kivutio huko Brazil


image
Kwenye mchezo dhidi ya Japan Fanny alikuwa amevaa jezi ya Balotelli
Kwenye mchezo dhidi ya Japan Fanny alikuwa amevaa jezi ya Balotelli
imageimage
imageimageimage image
Baloteli akishangilia goli alilofunga dhidi ya Japan.
Baloteli akishangilia goli alilofunga dhidi ya Japan.

Labels