50
Cent huenda akajikuta anakwenda jela miaka mitano na kutakiwa kulipa
faini ya zaidi ya dola 46000 ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 74 za
Kitanzania, kwa mashtaka matano aliyofunguliwa yanayotokana na tukio
alilofanya June 23 la kumpiga bibie Shaniqua Topmkins ambaye ni mama wa
mtoto wake.
|
Family Photo - Shaniqua, 50Cent na Marques |
Katika tukio hili, 50 Cent mbali na kumpiga Shaniqua, vilevile alifanya
uharibifu katika nyumba yake wa mali yenye thamani ya dola 7,100 zaidi
ya shilingi milioni 11 za kitanzania, ambapo vitu kama vile furnitures,
taa za mezani, TV na vinginevyo vilivunjwavunjwa, na msanii huyu aliondoka eneo la tukio muda mfupi kabla ya Polisi kukufika.
|
Huyu ni Mtoto wa 50 Cent, Marques anavyoonekana hivi sasa |
Kesi ya msanii huyu itaanza kusikilizwa June 22.
|
Shaniqua na mwanasheria wake |
0 maoni:
Post a Comment