Uhodari
wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya
kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana
kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na kisha wakamkata
kiganja cha mkono wa kushoto na kuanguka.
Kwa sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya.
Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake mkoani Mara kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya ndugu kutaka kuwanyang’anya bado vinaendelea.
Katika tukio lingine wilayani Bunda dereva mmoja wa pikipiki ameuawa na
watu wasiojulikana ambapo taarifa zinasema kuwa kabla ya kuuawa kwa
dereva huyo wa bodaboda inadaiwa alikodiwa na watu wawili.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea
kwa matukio hayo na tayari watu wanne wamekamatwa wakiwemo watu
wanaotuhumiwa kumkatakata mapanga mwanamke Sumayi Girandi.
0 maoni:
Post a Comment