Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, July 31, 2013

Baada ya Watanzania kukamatwa na dawa za kulevya, hiki ndio kimemkuta Madee akiingia Afrika Kusini

1
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com Madee amehadithia kila kitu kilichomtokea wakati anaingia tu Afrika Kusini siku kadhaa zilizopita ambapo hii imetokea kutokana na ukubwa wa habari, uzito wa tukio la wale Watanzania wawili wasichana waliokamatwa kwenye kiwanja cha ndege Johannesburg wakiwa na dawa za kulevya wakitokea Tanzania.
Madee anakwambia alipotua kwenye kiwanja cha ndege, kawaida huwa kuna utaratibu wa kuchekiwa hati ya kusafiria na ukaguzi mwingine ambao hufanywa na mitambo maalum kwa kila abiria anaeingia Afrika kusini, ni ukaguzi ambao unafanywa Airport kabla ya abiria kuruhusiwa kuingia kwenye nchi yenyewe.
Kilichomfanya Madee kusachiwa na kuhojiwa karibu dakika 60 ni pale tu aliposema anatokea Tanzania, kuna wazungu wawili wenye sare tofauti za kipolisi wakaanza kumsachi mpaka kufikia kumwambia avue t shirt yake, alivua t shirt na kubakiwa na nguo nyepesi ya ndani wakati huo abiria wenzake aliokwenda nao walikua wameruhusiwa.
Kati ya abiria wote waliokuja pamoja kwenye ndege, Madee na Mzimbabwe mmoja ndio walikaguliwa sana ila huyo mwingine alikaguliwa kidogo tu kama dakika 10 na wala hakuambiwa avue nguo.
Sehemu yenyewe Madee aliyoambiwa avue nguo sio kwenye chumba maalum, ni palepale kwenye foleni wanaposimama watu ila kwa pembeni kidogo, ni sehemu ambayo imezibwa na kioo kinacholingana na usawa wa tumbo kushuka chini…. Madee anakwambia jamaa walinong’onezana sana wakati wanamkagua.
Hata hivyo baada ya Askari hao kumuweka sana msanii huyu wa bongofleva kutoka kundi la TipTop Connection walimuomba radhi baada ya kumaliza ukaguzi wao ambao pia ulihusika kulivuruga sana begi lake.
Unataka kupata stori kamili? sikiliza AMPLIFAYA ya Clouds FM leo saa moja usiku, pia kwa Breaking News, habari yoyote ambayo ni habari, vituko, vichekesho, videos na music na mengine… jiunge kuwa mwanachama wa millardayo.com kupitia facebook https://www.facebook.com/millardayo au twitter https://twitter.com/millardayo pia instagram.com/millardayo ili uwe wa kwanza kutupiwa link kila tukio linapoandikwa.
2

Beyonce na Jay Z Wamtembelea Kim Kardashian na Mtoto Wake North West Nyumbani

 
Kwa rafiki wa kweli hata uwe bize vipi kujali huwa ni kitu muhimu!

Beyonce na Jay Z walitumia muda wao huku wakisitisha baadhi ya mambo ambayo waliyapanga kwenye ziara zao ili waweze kufanya kitu kioma cha msingi yumbani kwa Kris Jenner ndani ya Calabasas, Calif siku ya Jumapili July 28 lengo likiwa ni kumtembelea Kim Kardashian na mtoto North West, chanzo kimoja toka Marekani kimeeleza.

Imeelezwa pia Kanye hakuwepo nyumbani kwa muda huo (rapa huyo kwa sasa yupo ndani ya jiji la Milan, Italy), na kwa pamoja Jay na Bey walitumia muda wao asubuhi hiyo wakiwa na Kardashian, 32, ambaye hajaonekana hadharani toka alipojifungua mtoto huyo mnamo June 15.

Mwanamuziki Miley Cyrus Ajiachi Utupu kwa Ajili ya Kampeni



Miley Cyrus kupitia mtandao wa Twitter mnamo siku ya Alhamisi usiku alizungumzia juu ya kolabo lake na Marc Jacobs kwenye kampeni ya Linda Ngozi yako, kampeni ambayo inahusika na kukusanya hela kwa ajili ya Taasisi ya Kansa ya Chuo Kikuuu cha New York.

 
Ni picha ambayo aliitumia kwenye tweet hiyo na taarifa hiyo ndiyo ambayo imeonekana kushika vichwa vya watu zaidi kutokana na mazingira yake.

Siku za karibuni nyota huyo amekuwa kwenye kampeni hiyo, ila picha iliyotumika kwenye T-shirt hiyo imekuwa ya utupu ikishindwa kuziba sehemu zake za kike.


Picha iliyotumika ku-tweet ujumbe wa Cyrus

 

OSTAADHI JUMA NAMUSOMA ALIAMUA KUIMBA ILI KUMKATA NGEBE MR. BLUE

 

Manager wa Kampuni na label ya Mtanashati Entertainment inayosimamia Wasanii kama vile Dogo Janja, PNC, Happy Balice na wengineo, Maarufu kama Ostaadhi Juma Namusoma ameamua kufunguka live kuwa Sababu ya yeye kuingia kwenye Muziki kwa upande wa Kuchana na kuachia ngoma yake aliyofanya na Young Killer haikuwa na maana ya kutaka tu kuonyesha kuwa anaweza pia upande wa pili bali pia nikumkata Ngebe Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue ambaye anadai kuwa alimdiss kwenye kipindi cha Mkasi wakati akihojiwa na Salama Jabir.

Ostaadhi Juma amefunguka hayo wakati akipiga short Interview kwa njia ya simu na Mtangazaji wa Mambo Jambo Radio Arusha DJ Haazu ndani ya Kipindi cha Mtaa wa Pili Round II ambapo bila kuficha Jamaa alifunguka maneno hayo ambapo anasema baada ya Mr. Blue kumdiss kwenye kipindi cha Mkasi kuwa haujui Muziki yeye hakujibu chochote.

Mr. Blue alimdiss jamaa huyo pale alipoulizwa na Salama Jabir kuwa angependa apate Manager wa aina gani ambapo Mr. Alimjibu Salama kuwa anataka Manager anayejua mziki na sio vimanager kama Ostaadhi sijui Juma....jamaa yeye alikaa kimya na kwa sasa Kaamua kufunguka


Tuesday, July 30, 2013

NEW SONG | ROTA F| RICH MAVOKO - WAJUE


LYRICS | STAMINA F| DARASA & WARDA - MWAMBIE MWENZIO


 

Artists:Stamina ft Darasa&Warda
Studio:One Love Fx
Producer:Tiddy Hotter
Song writers;sStamina(verses)Darasa(choruss)
Intro:(stamina)
stamina)……you what tiddy?this is one love fx,shorwebwenzi on this one,itc moro town beiiib
vers 1(stamina)
wakuja rudi bushi,mji unahitaji waliosoma.
Kicheche usikae uchi,huku umevaa sketi ya ngoma.
Safisha kope,braza mungu sio deusi.
We hushangai mzungu mweupe,ila ana kivuli cheusi.
Kuitwa lijali,ina maana nyumbani tule.
Ukimwi kuutibu aghali,sasa iweje uupate kwa bure.
Binti usitoe mimba,ukihisi utakosa soko.
Zaa umtunze kinda,mbinguni usichomwe moto.
Acha kuiba,we fisadi uliyetukuka.
Mstue na ngariba,nae aache watu wanakufa.
Dogo unayekunywa gongo,ukifa utazikwa la mboto.
Na denti skuli ndo mchongo,ya mjomba mwachie mpoto.
Teja pandisha mlege,rudisha kete kwa pusha.
Mwambie atanyea debe,akikamatwa na vya arusha.
Acha makuzi,mpendaji ili ufike mbali.
Mapenzi king’amuzi,na pesa ndo digitali.
Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)
Vers 2(Stamina)
Ewe mtegemea ndugu,mwenye mikono na miguu.
Umasikini tatizo sugu,kuliko hata mr II.
Baba la baba,weka ubaba kila level.
Kitaani usawa unakaba,hadi padri anaishi kwa devil.
Mabadiliko,daima huanza na wewe.
Kama unakokwenda siko,uliza ili usichelewe.
Mche mungu,kama hajapanga hajapanga.
Kama ridhiki mafungu,kwanini ushinde kwa mganga.
Kusoma mpaka uchizi,ni kukosa kujiamini.
Mvivu unayependa usingizi,utakufa ukiwa masikini.
Endapo utailaza akili,usitegemee shida kukuamsha.
Hakuna mpenzi kama dili,funga nae pingu za maisha.
Hakuna tofauti,kati ya tajiri na masikini.
Uvae bukta uvae suti,ila wote tutazikwa chini.
Msimtenge mkiwa,kisa wazazi wake walimtupa.
Hata ng’ombe ana maziwa,ila akila simu anakufa.
Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)
Vers 3(Stamina)
Huna hata cheti cha form 4,na una ndoto za kuwa raisi.
Nyumbani unajaza choo,hupaswi kungoja na urithi.
Kufeli hasara,akili hailetwi na milo.
Sio kisa dunia duara,ndo denti upate ziro.
Kila kitu kizuri,duniani huletwa na pesa.
Kwanza elimu haina umri,usiogope kusoma memkwa.
Ujanja hauna miaka,kiujinga we baki mdogo.
Acha uchu wa madaraka,kwa kuongoza hadi vigogo.
Hivi vifo vya wasanii,vinatokea kama ajali.
Ee mungu mshushe nabii,atukumbushe kusali.
Tumia akili,maishani uongoze jahazi.
Na usitafute utajiri,kwa kumtoa kafara mzazi.
hujachelewa bado,cha msingi we piga kago.
Shukuru bado unahema,wala usishushe vilago.
Kijana taifa la leo,usilale ijenge kesho.
Huu ukoloni mambo leo,usikufanye ujione special.
Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)
Outro(warda)
Mwambie mwenzio (mwambie mwenzio)x4

Makomando Waingia Katika Vita Kali Na Ali Kiba

Kama unakumbuka miezi flani iliyopita Kundi la Makomando lilitambulisha style ya dancer maarufu kama Kibega na baadae tulisikia kuwa ni style ya bendi nyingine hapa Tanzania.

Well kitu hiki kimetokea tena. Sasa ni Makomando na Ali Kiba.

Nimefanya Exclusive interview na Makomando kupitia sammisago.com, wamefunguka kuhusu style yao mpya ya kucheza ya Ki-BabaBaba inayochezwa kwenye Wimbo wao mpya wa Ki-BabaBaba. 

Makomando wamesema tayari Msanii Mwenzao Ali Kiba amewapigia simu nakusema hii style ni yake na hataki waitumie. Kwa mujibu wa Makomando wamesema Ali Kiba amewauliza kwanini wametambulisha style yake ya kucheza na kuwa dancers wa Kiba [ 4 Real Dancers ] ndio wamewafundisha Makomando style hio.

Makomando wapo kwenye harakati za kusajili style hii mpya ya KiBabababa leo au kesho, wanataka kusajili Basata ili Msanii au bendi yoyote isidai kuwa ni style yao.
Ali Kiba Amesema alipo Ona wanatambulisha style hio, alichofanya nikuwapigia simu nakuwa tahadharisha kuwa wanatumia style ya Dancer Wake na kuwa walikuwa na mpango wakuitumia kwenye video yake. 

Ali aliendelea kusema Makomando walimbishia na kusema Style hio ni yao, yameigundua na wameipa jina, waka mkatia Kiba simu.

Ali kiba amesema amekasirishwa na kitendo cha kubishiwa kuhusu style hio na kukatiwa simu na wasanii anao waona kama wadogo zake.

Fahamu Ali Kiba na Makomando wote wana mpango wakutumia style hio kwenye video zao.

TOP 20 | ORODHA YA NYIMBO 20 BORA ZA REDIO KITULO FM TAREHE 28 JULAI 2013.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjOXcqEx68IUqTVFh0S5aTmLshQmA8m7GA3R_ZRlFoSrHIZUz94xp5KWlvNrC3xGorAbemCf5gYyReCt0bTm7PUS2aOuHZPxgxqTgD7X0X2-a_tphFJJuspJ-b5B056M6PnTk1z5v_viA/s1600/top+20.jpg

Nafasi wiki hili
Jina la Wimbo & Msanii
20
Mpenzi – Bonnie Valentino [Ingizo Jipya]
19
Bila Kukunja Goti – AY & Mwana FA F| J Martins [19 For 2 weeks]
18
Muziki Gani – Nay Wamitego F| Diamond [17 For 2 weeks]
17
Kama Huwezi – Ramadee F| Lady JayDee [20 Last week].
16
Watu – Tiko [17 Last week]
15
Sina Makosa – Timbulo [09 Last week]
14
Mwali Kigego – Rachel [14 For 2 weeks]
13
Masebena – Y Tony [12 Last week]
12
Wanipa wazimu – Lawize Entertainer F| Ney Lee The Super Nyota [10 Last week]
11
Yahaya – Lady JayDee [16 Last week]
10
Sina Imani – Shetta F| Rich Mavoko [10 For 2 weeks]
09
Thanks God – Godzilla a.k.a ‘zizi’ F| Walter [15 Last week]
08
Jikubali – Ben Pol [08 For 2 weeks]
07
Furaha ya Leo – Dream [07 For 3 weeks
06
Uzuri wako – Jux [04 For 2 weeks]
05
Riziki yangu – Linex The V.O.A F| Wayre [04 Last week]
04
Attention – M Rap F| Deddy [05 Last week]
03
Love Me – Izzo B F| Barnaba & Shaa [03 For 3 weeks]
02
Rest Of Ma Life – Hemedy F| Mr Blue [02 For 3 weeks]
Bonus Track
DUNIA INAMVUTO – AD
01
Jitunze – Mr R.E.D [01 For 2 weeks]

ORODHA YA NYIMBO 20 ZA REDIO KITULO ZIMEANDALIWA NA:-
Ergonelly The Pitch Controler.
PRODUCTION IMESIMAMIWA NA:-
DJ NUNDU THE ONE & ONLY
MAONI | USHAURI | PENDEKEZO |KURA TUTUMIE KUPITIA
Email:-ergonsanga@yahoo.com AU
kitulofm@yahoo.com
SIMU:-+255 718 742 990
Keep Entertained.
Imedhaminiwa na ELLY BLOG.

Labels