Unamkumbuka Wabogojo? Sasa anakula show za kimataifa, yupo kisiwa cha mahela, Macau, amshukuru Mr Nice japo alikuwa hampi hela nzuri
Mara ya kwanza kumfahamu Athman Ford "Wabogojo" ni pale nilipotizama
video ya wimbo wa Mr Nice unaoitwa "Kikulacho"...alikuwa anafurahisha
sana kwa vitendo vyake ambavyo ni vya kuchekesha na kushangaza kwasababu
si kila mmoja wetu anauwezo wa kufanya alichokuwa akikifanya.
Baada ya kuonekana kwenye video hiyo, Wabogojo akaanza kujulikana na hatimae kupata mashafu mpaka nchi za duniani "Europe"
"Kwaufupi!!Baada
ya Ziara ya Europe na Mother africa show ambayo tulipelekwa na Winston
Ruddle!! Bwana Winston pia akafanikiwa kutupatia Kazi nyingine ambayo
ndio hii ya sasa!!
Mazoezi ya hii shoo tulifanya kuanzia feb 2009 hadi march 2010 pale Belgium Antwerpen Centre baada ya hapo ndio tukaja huku Macau na kuandaa show.
Show tukaanza mwezi 17 Sept 2010 na Mkataba ni Mzuri na Tunalipwa pesa nzuri kwa Mwezi hadi rahaaaa!!Tutakuwa huku hadi Sept 2014 au Zaidi ya hapo inategemea kama utapewa Mkataba Mpya au Kama Umechoka pia ni Uamuzi wako na wao pia!!"
"Tupo Watanzania 12 katika hii show wengine wote nchi za America,Brazil,Uk,USA NK
Macau ni
Kisiwa kipo Asia, Chenye Macasino mengi sanaaa huku watu huja kutumia
helaaaa tuuu na Ku gamble, kama Las Vegas USA, na sisi show yetu ipo
katika Moja ya Cassino kuuubwa linaitwa CITY OF DREAM na Show yetu
yaitwa The House of Dancing Water."
" Mambo mengi tumejifunza Kuogelea na Scuba Diving pia maana kama hujui kuogelea basi hii show haikufai.
Namshukuru Sana Mr Nice japo kuwa hakuwa ananipatia pesa nzuri,Lakini nilichokipata ni zaidi ya pesa!
Mungu yu mwema!!"
kama ulikuwa
hujui, wabogojo ni kaka yake producer Razak Ford, (4D videos)
alietengeneza video ya Recho "Upepo", na pia ni kaka wa muigizaji wa
bongo movie "Shamsa Ford)
0 maoni:
Post a Comment