Pages

Saturday, July 06, 2013

Wakati 50 Cent akiwa anatumia nguvu nyingi kujisafisha na tuhuma za kumpiga Mama Mtoto wake, Huyu ndiye Model aliyejitokeza hadharani na kusema kuwa yeye ndiye aliyeshambuliwa na rapa huyo mwezi uliopita

Kufuatia tuhuma za 50 Cent kumpiga Mama wa Mtoto wake [Shaniqua Topmkins] ambazo zimevuma sana kwa wiki hii ambapo pia rapa huyu ametumia nguvu nyingi sana kuzikanusha, Sasa mapya yameibuka baada ya Girlfirend wa msanii huyu ambaye wengi walikuwa hawamfahamu, Bibie Daphne Joy ambaye ni model kutoka Philipines kuibuka na kudai kuwa yeye ndiye mwanamke ambaye 50 aliingia katika ugomvi naye mwisho wa mwezi uliopita.
Daphne Joy
Mwanadada huyu kwa mujibu wa ripoti pia ameweka wazi kuwa, ana mtoto mmoja na 50 Cent na kwa sasa lengo lake kubwa ambalo anazingatia ni kuwa salama yeye pamoja na mtoto wake.


50 Cent kwa sasa amewekeza nguvu nyingi pamoja na wanasheria wake kujisafisha na kufanya uchunguzi juu ya chanzo cha tuhuma hizi ambazo kwa mujibu wake hazina ukweli wowote.

0 maoni:

Post a Comment

Labels