Pages

Monday, September 17, 2012

Beyonce ashangazwa na jinsi watu wanavyomsema vibaya mwanae



Beyonce akiwa na mwanae Blue Ivy wakati walipokuwa likizo nchini Ufaransa hivi karibuni

Beyonce anadaiwa kushtushwa na maoni yanayotolewa na watu kwenye mtandao kuhusu binti yake Blue Ivy.
Muimbaji huyo amekuwa akifanya mambo chini chini tangu ajifungue mtoto wao wa kwanza na mume wake Jay-Z January 7 mwaka huu, lakini amekuwa akifuatilia namna watu wanavyoizungumzia familia yake.

Wanandoa hao walipost online picha za kwanza za Blue wiki iliyopita ambapo pamoja na kuwepo na maoni ya watu wanaoitakia heri familia hiyo, kumekuwepo na maoni yasiyopendeza dhidi yao.

“Someone better kill off that baby,” mtu mmoja aliandika kupitia Twitter huku mwingine akisema: “What an ugly-ass baby.”

Bey na Jay pia wamekuwa wakishambuliwa kiubaguzi wa rangi na chanzo kilicho karibu nao kimesema wanashangazwa na jinsi baadhi ya watu wanavyowachukulia.
 
“BeyoncĂ© is horrified by all the hate. 

It ranges from racism and foul language to questioning who the father is. Luckily there have been loads more saying how beautiful the baby is,” kilisema chanzo hicho.

0 maoni:

Post a Comment

Labels