Pages

Wednesday, September 12, 2012

KAULI YA H BABA KUHUSU IRENE UWOYA KUHARIBU UJAUZITO, MZEE MAJUTO NA MKWARA WA KULOGA MTU, VIKO HAPA


.
U heard na 255 nni segment za stori za town ambazo husikika kwenye show ya XXL Clouds Fm kuanzia jumatatu mpaka ijumaa saa saba mchana.

Stori kutoka U heard ya september 11 2012 Soudy Brown ametiririka na kuongea na msanii wa filamu Tanzania Mzee Majuto kuhusu kuibiwa na kupiga mkwara wa kumloga mtu aliemuibia.

Siku zote huwa nikimsikia Mzee Majuto anaongea ni lazima nicheke, kumsikia mwenyewe akizungumza kuhusu waliomuibia… bonyeza play hapo chini.
.
Stori za 255 na Miss Info Doreen Andrew ni pamoja na kauli ya H baba kuhusu kuwachana wasanii wenzake, pia kuhusu chanzo cha kuachana na mpenzi wake wa zamani ambae ni Irene Uwoya aliedaiwa kusema kwamba katika wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi, H Baba ndio alikua mbovu kuliko wote kwenye mapenzi, hajui chochote.

Kuhusu hilo H baba amejibu kwa kusema chanzo cha yeye kuachana na Irene ilikua ni baada ya kumpa ujauzito ambapo siku moja walikwenda hospitali kutokana na Irene kujisikia vibaya lakini walipofika hospitali Irene ambae aliingia kwa dokta peke yake aliutoa huo ujauzito bila kumpa H baba taarifa kabla, wakati walikwenda wote hospitali, H baba hakukubaliana na hiyo ishu na kuanzia hapo ndio kila mtu akashika njia yake.

0 maoni:

Post a Comment

Labels