Pages

Saturday, September 01, 2012

MSHINDINI WA BSS ATARAJIA KUZINDUA ALBAMU



Mshindi wa wa mashindano ya Bongo Star Search (BSS) 2009 Pascal Cassian anatarajia kuzindua albamu yake ya nyimbo za injili ya Yasamehe Bure kesho Uwanja wa Fisi , albamu hiyo itakuwa na nyimbo za Chuki ya Nini, Nikumbuke na Mimi, Jina la Yesu ,Mafuriko, Pesa ,Baba na Usilie

Akizungumzia albamu hiyo alisema kuwa ina lengo la kuwarudisha waliopote kwa mungu kwa kuwapatia ujumbe wa neon la mungu kwa njia ya nyimbo za mungu, alisema akiwa kama kijana ameamua kumtumikia mungu nguvu na akilizake nyingi katika kumuimbia na kumsifu mungu na hivyo amewataka kuwafikishia vijana watoto na watu wazima ujumbe huo kupitia nyimbo hizo

Pia akizungumzia sababu ya kuzindua albamu yake katika eneo la Uwanja wa Fisi alisema kutokana na sifa mbaya ya eneno hilo ambalo lilikuwa likifahamika kama uwanja wa dhambi kutokana na matukio mbalimbali ambayo ynafanyika mahali hapo Alisema mgeni rasmi anatarajia kuwa jaji Mkuu wa mashindano ya EBSS Ritha Paulsen ambaye ndiyo aliibua kipaji chake kupitia mwaka 2009 wakati yakiitwa BSS
 
Na Pro -24

0 maoni:

Post a Comment

Labels