Pages

Saturday, September 01, 2012

MPOTO ATAKA WABEBWE ILI WAFANIKIWE



Msanii wa Muziki wa Mashahiri Mrisho Mpoto maarufu kama Mjomba amewataka watanzania na kampuni yanayowapa nguvu ya kutoka kimuziki kutowaacha njia panda badala yake wawabebe hadi wafanikiwe

Akizungumza dare s Salaam juzi Mjomba alisema kasumba ya watanzania kupenda vitu vipya kila wakati haiwezi kuupeleka muziki popote

“Cha msingi hapa wanatufanya tupae kimuziki wanatakiwa kuhakikisha tunafanikiwa ndipo waanze na wengine lakini si kutuacha njia panda tunaelea halafu wakawachukua wasanii wapya na kufanya hivyo hakuwezi kufikisha popote tasinia ya muziki” alisema Mjomba

Aidha tofauti na hilo pia alikiri kwamba kuna wanamuziki wanaoibuka na wanafanya muziki mzuri, lakini amelaumu kwa wasanii wa tasinia hiyo kujitenga baadala ya kukaa pamoja na kubadilishana mawazo kama zilivyo nchi nyingine

Hata hivyo Mjomba alitamba kuwa mashairi mengi ambayo amekuwa akitoa ni mazuri ambayo yamekuwa yakiwafanya mashabiki kumpenda na kumwingizia kipato

0 maoni:

Post a Comment

Labels