Pages

Tuesday, September 18, 2012

Dogo Janja abadili jina, sasa ni JANJARO



Jumamosi ya September 15, 2012 msanii aliekuwa Tip top na sasa akiwa chini ya Mtanashati entertainment aliyefahamika kama Dogo Janja, alisheherekea birthday yake na alikuwa anafikisha umri wa miaka 18 ambao sasa unamuweka katika kundi la watu wazima.

Kutokana na hilo Mmiliki wa kundi la Mtanashati Ostadh Juma na Musoma ambae ndio msimamizi wake kwa sasa, kupitia kipindi cha Power Jam cha East Africa Radio leo Jumatatu 17th Sept 2012, amesema sasa msanii huyo hataitwa Dogo Janja tena bali jina rasmi atakalotumia ni JANJARO.

Juma na Musoma ameongeza kuwa huo ni uamuzi ambao ulifanywa na Mtanashati kwa kushauriana na Dogo Janja mwenyewe na jina hilo limeanza kutumika rasmi siku hiyo aliyotimiza miaka 18.

Historia inaonyesha kuwa wasanii wengi duniani ambao huwa wanaanza muziki katika umri mdogo sana, huwa wanaanza kwa kutumia majina yanayoashiria udogo wao na baadae huwa wanakuja kuyabadili majina hayo, hasa wanapofikisha umri wa kuwa watu wazima yaani miaka 18.

Baadhi ya wasanii waliowahi kubadili majina yao ni pamoja na Bow wow ambaye hapo kabla alikuwa anatumia Lil Bow wow, mwingine ni Romeo ambaye kabla ya kubadili alikuwa akitumia Lil Romeo.

Kwa hapa bongo tukiachilia mbali Janjaro ambae kabla alikuwa Dogo Janja, mwingine ni Dogo Hamidu ambaye kwa sasa anatumia Nyandu Tozi, na Ditto ambaye hapo mwanzo alikuwa anatumia Dogo Ditto. 

Msanii mwingine ambaye mpaka sasa anatumia jina lake kutokana na umri wake mdogo ni Yule kutoka mwanza anaitwa Dogo Baraka.

0 maoni:

Post a Comment

Labels