Pages

Sunday, September 16, 2012

NICKI MINAJ AJIINGIZA KWENYE SIASA KWA KUMFAGILIA ROMNEY



Nicki Minaj alishambuliwa na baadhi ya mashabiki wake baada ya wimbo wake mpya alioutunga kwenye albam ya nyimbo mchanganyiko ya ‘Lil Wayne ya Dedication 4’kumsifu mgombea urais Mitt Romney

“Mimi ni Republication nampigia kura Mitt Romney “Nicki Minaj alirap verse ya wimbo uitwao ‘Mercy’

Kwa mara ya kwanza rais Obama amezungumza moja kwa moja kuhu wimbo huo wakati wakiwa katika kampeni mjini Florida, Rais alizungumza na watangazaji Obie na Lil Shwan wa kipindi cha ‘Morning Show’ cha redio Powe r 95.3

“Sina hakika kama jambo hilo limetokea “rais Obama alisema ‘nadhani ameweka wimbo wake mle, ameweka mistari michache ya rap , lakini anapenda kutoa kivingine hivyo sijui nini kinachoendelea pale “

Baada ya kusikia mahojiano hayo Nicki Minaj mara moja alitumia ukurasa wake wa Twitter kumshukuru rais kwa kuelewa rapa yake

“Ha asante sana kwa kuelewa ubunifu wangu Bw. Rais , wajanja daima hutambua ukweli natuma upendo na sapoti kwa Barack Obama “ Nicki Minaj aliandika

0 maoni:

Post a Comment

Labels