Pages

Monday, September 24, 2012

LADY GAGA AMZIMIKIA MWANAMITINDO WA BONGO









Mwanamitindo maarufu nchini Flaviana Matata ameendelea kung’ara katika fani hiyo baada ya kung’ara katika maonesho ya wiki ya Mavazi ya London, ‘ London Fashion Week’Fraviana ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani kwa shughuli hizo za mavazi, aliwavutia sana wadau wa maonesho hayo hasa mwanamuziki nyota wa kike duniani Stefani Joanne Angelina Germanotta maarufu kwa jina la Lady Gaga
Mwanamitindo huyo anawasisimua wadu wengine wa mitindo wakiwemo watu maarufu duniani na kuendeleza kujizolea sifa na kutangaza jina lake na nchi yake pia, Fraviana amekuwa akishiriki maonesho hayo tangu mwaka 2010 , hata hivyo mwaka huu ameonesha kukomaa zaidi na kuweza kutawala jukwaa hilo

Maonesho ya mavazi mwaka huu yaliwahusisha wabunifu wengine wengi maarufu wa mitindo ambapo mmoja wapo ni Vivenne Westwood Red Label ambaye anatamba duniani, pamoja na kuwepo kwa mbunifu Philip Treaacy naye alifanya mambo makubwa kwenye maonesho hayo yaliyozinduliwa na Lady Gaga

Flaviana alipewa heshima kubwa ya kuvaa jaketi la mwanamuziki aliyekuwa mfalme wa muziki wa aina ya Pop Marehemu Michael Jackson pia livaa mavazi ya wabunifu maarufu kamamMike Fast na Christopher Raeburn

0 maoni:

Post a Comment

Labels