Pages

Sunday, September 16, 2012

WASANII WASHAURIWA KUJIHESHIMU



Wasanii washauriwa kujiheshimu na kuwa na heshima juu ya kazi zao za sanaa ya muziki ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea

Skendo za kila siku kwenye baadhi ya vyombo vya habari haziwezi kumjenga msanii katika soko la muziki la kimataifa bali inachangia kumboboma na kuvunja heshima yake kwa wadau na mashabiki wake wa muziki

Wasanii wanatakiwa kuwa na uongozi utakao waongoza na kuwapa mafunzo nini maana ya sanaa ili waweze kuheshimu kazi zao

Kauli hiyo ilitolewa na msanii anayetikisa katika anga za muziki wa kizazi kipya nchini Barnabas Elias ‘Barnaba’alipokuwa akieleza kuhusu uzinduzi wa staili yake mpya ya uimbaji inayoambatana na muonekano wa mavazi pamoja na aina ya nywele

Alisema kuwa mashabiki wake watarajie kumuona Barnaba wa tofauti kuanzia mavazi mpaka uimbaji hii yote katika kuboresha kazi ili zionekane zina ubora

Aliongezea kuwa kwa kuwa anaheshimu kazi zake pamoja na kuwajali mashabiki wake hufikiria vitu vyenye ubora zaidi katika kazi zake

0 maoni:

Post a Comment

Labels