Ile track ya ''Kama Zamani'' kutoka kwa rapper Mwana FA ambayo ameshirikiana na Kilimanjaro Band [Wananjenje] pamoja na Man'dojo na Domokaya ambayo ilitakiwa kutoka leo imeahirishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.
Lifeline Music Inc. ndio kampuni inayosimamia kazi
zote za rapper huyo, na ndiyo iliyotoa taarifa hizo za kuahirisha kwa
uzinduzi wa ngoma hiyo kwa sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao.
Soma taarifa kamili hapa chini:
TAARIFA KWA WADAU
Leo tarehe 25 Februari mwaka 2013 ndio ilikuwa iwe siku nyingine ya
kihistoria katika medani ya muziki wa kizazi kipya. Kwa siku kadhaa
sasa tumekuwa tukitangaza kwamba wimbo mpya wa MwanaFA ulio katika
mahadhi ya Hip Hop uitwao “Kama Zamani” aliowashirikisha Man'dojo,
Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wananjenje) ungeanza kuuzwa kupitia
njia mbalimbali kama ‘iTunes’, ‘Amazon’ na kupitia katika simu za
mkononi.
Pia ndio tarehe ambayo Kama Zamani ingeanza kusikika katika vituo vya redio Tanzania na nchi za jirani.
Lifeline Music Inc. ndiyo inayosimamia muziki wa
MwanaFA kwa sasa, ikiwa ni kampuni ambayo inafanya kazi za muziki,
kuangalia na kuhakikisha kwamba wasanii inaowasimamia wananufaika kwa
kiasi kikubwa kutokana na kazi zao; na kwamba muziki unaofanyika kwa
sasa unafuata kanuni zote zinazosimamia makubaliano ya biashara.
Kama mjuavyo, biashara yoyote ina pande mbili na mafanikio yake
yanategemea zaidi maridhiano baina ya pande hizo na utimizaji wa
vipengele tofauti ndani ya mikataba ya biashara.
Katika kuboresha maslahi ya wanamuziki husika na wimbo huu
piakuboresha zaidi njia zitakazotumika kuhakikisha ya kwamba burudani
hii itawafikia washabiki wengi zaidi wa muziki unaofanywa na MwanaFA,
Kilimanjaro Band(WanaNjenje) na Man’Dojo na Domokaya, tumefikia uamuzi
wa kusubiri na kusogeza mbele siku ya kuachia wimbo wa Kama Zamani kama
ilivyopangwa hapo awali.
Tunachukua nafasi hii kuwaomba radhi mashabiki ambao mmekuwa
mnasubiri kwa hamu kusikia ni nini muungano huu wa muziki wa kizazi
kipya na moja ya bendi kongwe kabisa za muziki yenye miaka zaidi ya 40
katika tasnia ya muziki Tanzania umewaandalia.
Kwa niaba ya MwanaFA, uongozi wa Lifeline Music Inc.
unaomba uvumilivu na subira toka kwenu mashabiki na wapenzi wa muziki.
Tunaamini kwamba subira huvuta heri na mambo mazuri hayahitaji haraka.
Tunawashukuru kwa dhati kwa ushirikiano wenu.
Henry Mkumbukwa
PR Strategist
Lifeline Music Inc.
Fans wengi wamekuwa wakiisubiri track hii kwa hamu, tumekuwa
tukiombwa links na wengi wakiiulizia kwa shauku ya kuusikia, Lifeline
Music wamezungumza na kuweka bayana kilichotokea.
I think its a good deal they are trying to pull through, tusubirie
tuone lini itatoka. As we promised ikitoka tu utaipata hapa hapa...
MAMBO MAZURI HAYATAKI HARAKA... Lol.. One!!
0 maoni:
Post a Comment